Home Kitaifa RASIMU YA MITAALA MIPYA NA RASIMU YA MAPITIO YA SERA KUKAMILIKA DISEMBA...

RASIMU YA MITAALA MIPYA NA RASIMU YA MAPITIO YA SERA KUKAMILIKA DISEMBA 2022-WAZIRI MKENDA

Na Mathias Canal

Serikali imesema kuwa imeamua kufanya mageuzi ya elimu ambapo kufikia mwezi Disemba 2022 rasimu ya Mitaala mipya pamoja na rasimu ya mapitio ya sera itakuwa imekamilika.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 25 Julai 2022 wakati akizugumza kwenye jopo la mjadala katika kikao cha Kikosi kazi cha Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya elimu Duniani uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Serikali ya Tanzania imejipanga vyema na kufikia Mwezi Januari mwaka 2023 inatarajia kuanza mchakato wa kufanya maamuzi baada ya Rasimu hiyo kuwa imekamilika.

Pamoja na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe Prof Adolf Mkenda mkutano huo pia umehudhuriwa na Waziri wa Elimu wa Namibia Mhe Ester Anna Nghipondoka, Naibu waziri wa Elimu, Bosnia na Herzegavina Mr Adnan Husic, Mkurugenzi wa Idara ya Masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa na Katibu wa Tume ya Kitaifa ya Elimu ya Qatar ya Utamaduni na Sayansi Mr Ali Al-Marafi.

Mchakato wa magezi ya elimu nchini Tanzania ulitokana na maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 22 Aprili 2021 kuhusu mabadiliko ya Mitaala ya elimu na muelekeo mpya katika sekta ya elimu aitakayo.

MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!