Home Kitaifa PROF. KITILA MKUMBO AVUNJA UKIMYA TAHARUKI YA UTEKAJI WATOTO

PROF. KITILA MKUMBO AVUNJA UKIMYA TAHARUKI YA UTEKAJI WATOTO

Katika siku za Karibuni kumekuwa na wimbi la upotevu wa watoto katika maeneo mbalimbali nchini huku wakidaiwa kuwa wanatekwa na watu wasiojulikana jambo ambalo limemuibia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo na kutoa tamko.

Akiwa ziarani katika Kata ya Makurumla iliyopo kwenye Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo amewataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki na Wazazi kuwalinda watoto wao wakati wote.

“Leo asubuhi (jana Jumatatu) tumeamka na taharuki katika Kata ya Makurumla na Mburahati kuwa watoto wametekwa mashuleni, tumetoa taarifa kwa vyombo vya dola jambo hili linafanyiwa kazi, uchunguzi ufanyike na jambo hili likomeshwe” Prof. Kitila Mkumbo.

Prof. Kitila amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha Kwa vyombo vya dola ili jambo hilo lidhibitiwe kama lipo wahusika wachukuliwe hatua na kama ni taharuki tu nayo ijulikane na hali ya kawaida iendelee.

“Nchi nzima hii kuna jambo la kuteka watoto wadogo linasikika, Kuna kaupepo ka kishetani kanaendelea hapa, tuchukue tahadhari, inavyoonekana siyo kama zamani wakati tukikua Sisi, mtoto alikuwa wa kijiji na mtaa lakini sasa hivi mambo yamebadilika, kuna watu wachache katika jamii yetu kwa kuwa na tamaa aidha ya kupata Mali mali kwa njia za mkato wanateka watoto, kila mtu amlinde mtoto wake” Prof. Kitila Mkumbo.

Mbunge huyo ambaye ndiye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji amewataka wananchi kila mmoja kwa imani yake aliombee Taifa ili hili jambo lisiendelee na hali katika jamii iwe ya utulivu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!