Home Kitaifa PROF. KITILA MKUMBO ATOA ZAWADI YA MWISHO WA MWAKA KWA WAKAZI WA...

PROF. KITILA MKUMBO ATOA ZAWADI YA MWISHO WA MWAKA KWA WAKAZI WA MABIBO

Waziri wa Nchi OR-MU na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo amesema kivuko cha waenda kwa miguu cha Sahara kilichopo Mabibo Dar es Salaam kitaanza kujengwa mapema mwaka 2024.

Akiwa katika ziara kwenye Kata ya Mabibo Prof. Kitila Mkumbo ametembelea mto Gide kwenye mtaa wa Mabibo na kukuta changamoto ya mawasiliano baina ya wakazi hao pindi mvua zinaponyesha huku kukiwa na taarifa za baadhi ya Wananchi kusombwa na maji na kuamua ujenzi ufanyike.

Baada ya kuona changamoto hiyo na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo amesema kwa kuanzia atatoa Sh. Milioni 10 ya mfuko wa Jimbo huku Halmashauri nayo ikitoa Sh. Milioni 20 ambazo zitaanza ujenzi mapema mwaka 2024 wakati fedha nyingine zikiendelea kutafutwa kwaajili ya kukamilisha ujenzi huo.

Changamoto kubwa katika Jimbo la Ubungo kipindi hiki cha mvua ni mafuriko kila kona hali inayosababisha miundombinu kuharibika ndiyo maana kila Kata ninayopita lazima kuwe na changamoto ya kivuko hivyo msiwe na wasiwasi kivuko hiki kitaanza kujengwa ili kuwapunguzia machungu Wananchi hasa nyakati za mvua ” Prof. Kitila Mkumbo.

Awali kabla hajafika kwenye kivuko hicho Waziri Prof. Kitila Mkumbo ametembelea kivuko kinachowaunganisha wakazi wa Mabibo na Manzese maarufu kama daraja la nyoka na kuahidi kuwa kitakarabatiwa.

Amewapongeza wakazi wa eneo hilo kwa kuwa na utamaduni wa kufanya usafi kwenye mto na kuahidi kushirikiana nao katika usafi huo kwa kuwapatia vifaa vya usafi.

= = = = = = =

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!