Home Kitaifa PROF. KITILA MKUMBO ATOA KITITA CHA SH. 2,000,000 KWA MASHABIKI WA SIMBA...

PROF. KITILA MKUMBO ATOA KITITA CHA SH. 2,000,000 KWA MASHABIKI WA SIMBA NA YANGA MAKURUMLA

Na Ofisi ya Mbunge Jimbo la Ubungo

Utani wa Jadi baina ya Simba na Yanga siyo uadui, ili kudhihirisha hilo mashabiki wa Vilabu hivyo katika Kata ya Makurumla kwa nyakati tofauti wamekutana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo.

Akiwa Makurumla Prof. Kitila Mkumbo ametoa kitita cha Sh. 1,000,000 kwa mashabiki wa Club ya Yanga na Sh. 1,000,000 kwa mashabiki wa Club ya Simba ambapo pia amepata Heshima ya kufungua Tawi la Simba.

“Katika historia yangu sijawahi kupata heshima ya kufungua Tawi la Simba, hili ni la kwanza hivyo nawaunga mkono katika masuala ya michezo ambayo huunganisha watu wengi” Prof. Kitila Mkumbo.

Prof. Kitila amesema ataanzisha mashindano ya mpira wa miguu baina ya mashabiki wa Simba na Yanga ndani ya Jimbo la Ubungo ambayo yataanzia kwenye ngazi ya Kata na badae kumpata Bingwa wa Jimbo la Ubungo.

Pamoja na kitita cha Sh. 1,000,000 alichotoa Kwa kila timu, Prof. Kitila Mkumbo ameahidi kuwatafutia ofisi mashabiki hao wa Timu za Simba na Yanga Kata ya Makurumla na Manzese.

= = = = =

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!