Waziri wa Nchi OR-MU na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo ameahidi kujengwa kwa baadhi ya barabara korofi kwenye eneo la Kilungule A ikiwemo barabara ya Msikitini – Kwa Puluku na Sadani – Kivulini ambazo mvua zikinyesha huwa hazipitiki.
Prof. Kitila Mkumbo pia ameahidi ujenzi wa vivuko katika baadhi ya maeneo yenye mito kwenye mtaa wa Kilungule A na Kilungule B Kata ya Kimara Dar es Salaam.
Akiwa ziarani katika mitaa ya Kilungule A na Kilungule B Kata ya Kimara Prof. Kitila Mkumbo ametembelea makazi yaliyoathiriwa na mto Gide na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo.
Katika ziara hiyo Mhe. Kitila amesikiliza changamoto za Wananchi ikiwemo kutofikika kwa baadhi ya maeneo nyakati za mvua kufuatia kukosekana kwa vivuko.
Kufuatia changamoto hizo Prof. Kitila amesema baadhi ya maeneo ambayo ni kikwazo cha Mawasiliano ikiwemo kivuko cha kwa Lyimo na kivuko cha Mfugale Kitonga.
Akiwa ziarani Prof. Kitila Mkumbo ameshuhudia uharibifu wa miundombinu uliosababishwa na mvua za El-nino na baadhi ya nyumba zilizoathirika.
Katika hatua nyingine ameahidi kujengwa kwa kingo za mto Gide katika maeneo korofi huku akiwataka wananchi wanaoishi maeneo hayo kuchukua tafadhali.
=======