Home Kitaifa PROF. KITILA MKUMBO AAHIDI ARDHI YA KILIMO KWA BODABODA WA MABIBO

PROF. KITILA MKUMBO AAHIDI ARDHI YA KILIMO KWA BODABODA WA MABIBO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji na Mbunge wa Jimbo la Ubungo Prof. Kitila Mkumbo akiwa ziarani katika Kata ya Mabibo amekutana na waendesha pikipipiki na kuwaahidi kuwapatia ardhi kwaajili ya Kilimo.

Ahadi hiyo ya Prof. Kitila imetokana na ombi lililotolewa na Vijana hao la kutaka kupatiwa ardhi kwaajili ya kilimo ambapo amewasiliana na Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ili asaidie kupatikana kwa ardhi hiyo.

Pamoja na ahadi hiyo pia amewapatia kiasi cha Sh. 500,000 ikiwa ni mchango wake katika mfuko wao waliouanzisha ili kujikwamua kiuchumi.

“Kwa hapa Dar es Salaam waendesha pikipipiki tunawaita maofisa usafirishaji na tunawathamini sana, hebu fikiria siku moja hapa Dar es Salaam kusiwe na Bodaboda hali itakuwaje? Hawa watu wanaisaidia sana sekta ya usafirishaji” Prof. Kitila Mkumbo Waziri wa Nchi OR-MU na Mbunge wa Jimbo la Ubungo.

“Niwaahidi kwa niaba ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kuwa Sisi kama Serikali pale ambapo vijana katika nchi hii wanajipanga kujikwamua kiuchumi tutawashika mkono maana wanaisaidia Serikali na nitumie nafasi hii kutoa wito kwa vijana wote nchini waendelee kujishughulisha” Prof. Kitila Mkumbo.

Mbunge huyo ambaye ndiye Waziri mwenye dhamana ya Mipango na Uwekezaji amewataka Vijana nchini kuendelea kujishughulisha kila mmoja katika sekta yake.

= = = = = =

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!