Home Kitaifa PROF.ASSAD AONGOZA KONGAMANO TATHMINI UJENZI HOSPITALI YA KIISLAMU MKOA TANGA

PROF.ASSAD AONGOZA KONGAMANO TATHMINI UJENZI HOSPITALI YA KIISLAMU MKOA TANGA

Na Boniface Gideon -TANGA

Aliyekuwa Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za Serikali,Profesa Mussa Assad leo ameongoza kongamano la tathmini ya ujenzi wa Hospitali ya Kiislamu Mkoa wa Tanga lilioenda sambamba na sherehe ya mwaka wa Kiislamu 1446 A.H,
Hospitali hiyo inatarajiwa kujengwa kata ya masiwani katika eneo la tumbirini na itagharimu Sh.2.4 Bilion, inatarajiwa itakapokamilika itahudumia Wananchi kwakufuata Maadili ya kidini ambapo mgonjwa atahudumiwa na Daktari/muuguzi wa jinsia yake.

Profesa Assad aliwataka Waislamu kutoa michango kwa bidii ili ujenzi wa Hospitali hiyo ukamilike kwa wakati,

“niwaombe Waislamu wenzangu tujitokeze kuchangia hicho kidogo ulicho nacho,lakini pia kila mmoja wetu ajitathmini kutokana na ujenzi wake kusua sua kwa muda mrefu,ni lazima tujali na kulinda mali za mradi huu uweze kukamilika kwa wakati,kila mmoja wetu ahakikishe anachangia na anahamasisha wengine kuchangia alicho nacho ili tumalize kwa Wakati ifikapo mwakani”

kwaupande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri kuu Bakwata Sheikh Khamis Mtaka amesema endapo kila mmoja atajitoa ujenzi huo utaisha kwa wakati,

“Ubinafsi wetu ndio ambao umesababisha mpaka leo hii tushindwe kumaliza ujenzi wa Hospitali hii,naomba tushikamane na tuache mafarakano ili tutimize malengo yetu,mshikamano na umoja wetu utatufanya tufanikishe ujenzi wa Hospitali yetu kwa haraka” Aliongeza

Nae Mjumbe wa kamati ya ujenzi wa Hospitali hiyo,Hamad Kidege, amesema ujenzi wa Hospitali hiyo umechukua muda mrefu sana kutokana na kusua sua kwa michango nakwamba wamelazimika kuweka bahasha maalumu kwaajili ya michango lakini muitikio sio mkubwa hivyo amewaomba Waumini wote kujitokeza kwa wingi kuchangia ili ujenzi uendelee,

“Tulijenga msingi kama mnavyoona, lakini wezi wamevunja nguzo na kuchukua nondo 72, kiukweli kitendo cha nondo kuibiwa kumeturudisha nyuma sana,na tumeongea na mhandisi amesema ili kurejesha kwenye hali yake ni zaidi ya Sh.16 Million, kwahiyo tunatakiwa tujitoe kwa nguvu zote kwakila mmoja wetu” Alisisitiza Kidege

                   MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!