![](https://www.mzawa.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250213-WA0156-1024x683.webp)
Meneja wa Precision Air nchini Comoro,Mohamed Rajab Juma ameeleza kuwa safari za Shirika hilo nchini Moroni zinashika nafasi ya pili kwa faida kati ya safari zake zote.
Akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Comoro,Saidi Yakubu, Meneja huyo alieleza kuwa Comoro inashika nafasi ya pili kwa faida baada ya Nairobi katika safari zake zote na hilo linajitokeza kwa mwaka wa pili mfululizo sasa.
Aidha alieleza kwa kutambua umaarufu wa safari hizo hivi sasa Shirika la Precision linaleta ndege nchini Comoro mara nne kwa wiki na muda mwingi huwa zimejaa.
Aliushukuru ubalozi kwa ushirikiano inaoutoa kwa Shirika hilo na kueleza mipango ya usoni ni kuwa na ndege itakuwa inazunguka visiwa vyote vya Comoro.
Kwa upande wake Balozi Yakubu aliwapongeza Precision na kuwaomba waongeze nguvu pia katika kutoa huduma nafuu za usafirishaji wa vifurushi hususan bidhaa za chakula.
![](https://www.mzawa.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250213-WA0158-1024x683.webp)