Home Kitaifa POLISI KAGERA YA MSHIKIRIA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MKE WA MWENYEKITI BUKOBA

POLISI KAGERA YA MSHIKIRIA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MKE WA MWENYEKITI BUKOBA

Na Theophilida Felician, Kagera

Jeshi la Polisi Mkoani Kagera linamshikiria mtu mmoja aitwaye Paschal Kaigwa Mwenye umri wa miaka (21) mkazi wa kata ya Kishogo Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera kwa tuhuma za kutekeleza mauaji ya kikatili dhidi ya mama mmoja Hadija Ismail aliyekuwa ni mkazi wa Mtaa wa National Housing (NHC) Kata ya Rwamishenye Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

Akitoa taarifa ya kukamatwa kwa mtu huyo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake Manispaa ya Bukoba kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Kagera William Mwampaghale amesema kuwa Paschal alikuwa akisakwa na Jeshi hilo tangu tarehe 13 February mwaka huu baada yakutokea kwa mauaji ya mwanamke huyo Hadija Ismail Mke wa Mwenyekiti wa Mtaa Devid Dominck ambaye
Aliuawa kikatili majira ya saa 12 jioni akiwa nyumbani kwake.

Kamanda Mwampaghale amefafanua kuwa mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akiishi nyumbani kwa Mwenyekiti tangu mwezi wa 11 mwaka 2022 Baada kumuokota mitaani ili kumsaidia kutokana na ugumu wa maisha aliokuwa nao alivyomaliza kutelekeza unyama huo alitokomea na kuendelea kuishi katika vichaka kwa muda wote huo hivyo mnamo tarehe 19 /2/ mwaka huu majira ya saa 10:00 alitoka mafichoni akiwa na njaa kali iliyomusukuma kwenda kutafuta msaada wa chakula nyumbani kwa shangazi yake anayeishi mtaa wa Katotorwansi kata Kashai Manispaa ya Bukoba ambapo aliwakuta watoto wa shangazi yake huyo ambao wanamfahamu na walipomuona walipiga kelele majirani wakafika na kumkamata.

Hata hivyo ameongeza kwamba Jeshi hilo linaendelea kufanya mahojiano naye ili kubani nini chanzo kilichompelekea kumuua mama huyo na utaratibu huo ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Kamanda huyo amevishukuru vyombo vya habari kwa jinsi vilivyohabarisha umma tangu kutokea kwa tukio hilo kwani juhudi hizo zimechangia pakubwa katika kufanikiwa kumtia nguvuni kijana huyo.

Amehitimisha akisema kuwa matukio ya mauaji bado Kagera yanashika kasi hivyo ametoa wito akiwasihi na kuwataka wananchi kuachana na vitendo hivyo ambavyo havifai katika jamii huku akisisitiza kuwa wale wote wanaojichanganya kushiriki matukio ya namna hiyo mmoja hadi mwingine watadakwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Ikimbukwe kuwa mama huyo aliyekuwa na umri wa miaka 29 na mzazi wa watoto wawili mpaka umauti unamkuta alifanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo kubakwa sambamba na kupigwa na kitu kizito kichwani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!