Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Jana 30 Machi 2024 alimuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mazishi ya Askofu wa kanisa La New Life Gospel Community Church (NLGCC ) Jimbo la Mara Kaskazini Bi. Fransisca Mwita Gachuma ambaye pia ni mwenza wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (NEC) Ndugu Christopher Mwita Gachuma.
Mheshimiwa Majaliwa alisema Mheshimiwa Rais Samia suluhu Hassan ameguswa na msiba huo na ataendelea kuthamini na kutambua mchango mkubwa wa familia ya Gachuma kwa wananchi wa Tarime na Tanzania kwa ujumla.
Naye, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Chama cha mapinduzi kitaendelea kuyachukua mafunzo ya Marehemu ili kujiimarisha zaidi na kukijenga chama hicho.
Mazishi hayo yalifanyika katika Kijiji cha Komaswa Wilaya ya Tarime Mkoa wa Mara.