Home Kitaifa PBZ JIWEKEZENI MIFUMO IMARA KUMRAHISISHIA HUDUMA KWA WATEJA

PBZ JIWEKEZENI MIFUMO IMARA KUMRAHISISHIA HUDUMA KWA WATEJA

Na Magrethy Katengu

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Ally Suleiman Ameir ameitaka benki ya Zanzibar PZB kujiwekeza kwenye Mifumo mizuri Imara ya Ulinzi yenye kumrahisishia Mteja popote walipo.

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam wakati alipotembelea tawi la benki hiyo lilo katika maonyeaho ya Sabasaba ambapo amesema PZB benki ina miaka 57 tangu kuanzishwa kwake na wamekuwa wakitoa huduma hivyo kupitia maonyesho hayo wanatakiwa kuangalia washindani wao wale waliyoyaona wajitathimini na waendelee kutoa huduma.

Wafanyakazi wa benki ya PZB jitathiminini kupitia maonyesho ya sabasaba washindani wenu kwa yale mazuri mliyoyaona kwani nyie mnaaminika kote kuanzia Zanzibari na Tanzania na Mmetunukiwa tunzo na Suma ya utoaji huduma vizuri hivyo nawapongeza kwa kufanya vizuri” amesema Naibu Waziri Ally

Hata hivyo ameipongeza Benki hiyo kuendelea kutoa gawio kwa Serikali pensheni ya jamii,hivyo ametoa amesema Benki ya PBZ imekuwa na matawi yake nchi nzima kwa kutanua wigo wa utoaji huduma kwa wateja wake kuwasogezea pale wale walipo .

Naye Meneja wa Benki PZB tawi la Kariakoo Machano Haji amesema katika sabasaba hii wametoa huduma za kifenda kwa ITM na Dirishani na wengine wameweza kufungua akaunti zote ikiweno za watoto za wakina mama na wafanyakazi.

“Tumesogeza huduma zetu karibu na wananchi ikiwemo kuwapatia mikopo ya bishara, nyumba, viwanja, na mashamba hivyo tunawakaribisha sanaa kutembelea matawi yetu yalio karibu nao” amesema Naibu waziri

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!