Home Biashara PATA GB 1 BURE UKIPAKUA SUPER APP YA TIGO PESA ILIYOBORESHWA ZAIDI...

PATA GB 1 BURE UKIPAKUA SUPER APP YA TIGO PESA ILIYOBORESHWA ZAIDI , SOMA HAPA

 Na Mwandishi Wetu

Kadili siku zinavyozidi kusonga ndivyo teknolojia nayo inavyozidi kushika kasi na hapo ndipo Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo ilipoamua kuja kidijitali zaidi kwa kuzindua App ya kisasa kabisa ‘Super App’ ya Tigo Pesa ambayo itawarahisishia maisha watumiaji wa huduma za kampuni hiyo.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha amesema App hiyo imekuja kufanya mapinduzi makubwa ya kuwarahisishia na kuwaboreshea maisha watumiaji wa mtandao huo kwa kutumia App hiyo mpya.

Angelica amesema kampuni hiyo ndiyo iliyoanza kuja na App ya kufanya miamala ya Tigo Pesa miaka kumi iliyopita lakini pamoja na mafanikio ya App hiyo wameonelea waje na App yenye ubora zaidi inayoendana na kipindi hiki ukilinganisha na ile ya miaka kumi iliyopita.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!