Home Biashara ONYO LATOLEWA WAFANYABIASHARA WANAOPANDISHA BEI YA SUKARI KUWAJIBISHWA KISHERIA

ONYO LATOLEWA WAFANYABIASHARA WANAOPANDISHA BEI YA SUKARI KUWAJIBISHWA KISHERIA

Na Magrethy Katengu

Bodi ya Sukari Tanzania mewataka wafanyabiashara wanaouza na bei ya sukari isiyo halali kuacha mara moja kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Agizo Hilo limetolewa Leo Januari 18, 2024na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania Prof Kenethy Bengesi ambapo amebainisha kuwa Kuna baadhi ya wafanyabiashara wanauza sukari kwa bei isiyo halali na kupelekea wananchi kushindwa kumudu gharama ya bidhaa hiyo muhimu.

Bodi inatambua kuwa kila mkoa unatofautiana bei ya sukari hivyo Wafanyabiashara wanaopandisha bei kwa maslahi yao binafsi tofafauti na bei halali ya mkoa huo tukiwabaini hatutawaacha tutahakikisha tuwachukulia hatua kali za kisheria kwani hatupendi kuona wananchi wakilalamika juu ya bidhaa hii muhimu kupandishiwa bei holela” amesisitiza Mkurugenzi

Akizungungumzia uhaba wa sukari uliopo kwa sasa Profesa Bengesi amesema haliyo imetokana na kunyesha mvua za Elmino zilizoanza mwezi oktoba 2023 na kupelekea mashamba ya miwa kujaaa maji pamoja na miundombinu ya barabara kuharibika hivyo kushindwa kuvuna miwa iliyotakiwa kupelekwa kiwandani kuchakatwa sukari .

Mwaka huu tumezalisha tani laki tatu na arobaini na tano pekee Ambala hazitoshelezi lakini kawaida mahitaji huwa ni tani laki tano na ishirini na katika uzalishaji tunapenda malengo yetu ni kuzalisha tani laki tano na hamsini na tano ili tuwe na akiba ya sukari ya kutosha lakini kutokana Msimu huu wa mvua za Elimino tumeshindwa kufikia lengo ndiyo maaana tuna uhaba wa sukari” amesema Bengesi

Hata hivyo amebainisha Serikali imechukua hatua za kukabiliana na uhaba wa sukari kwa kutoa kibali kwa kuagiza sukari nje ya nchi tani elfu hamsini na kwama sukari hiyo inatarajiwa kuingia nchini januari 22 , 2024 .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!