Na Shomari Binda-Musoma
MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi ya CCM mkoa wa Mara Wilfred Nyihita amewataka vijana walio kwenye nafasi za uongozi wa umma kuwa wazalendo na waaminifu.
Akizungumza na Mzawa Blog ikiwa ni siku ya kimataifa ya vijana leo agosti 12/2024 amesema serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inawapa vijana nafasi za uongozi na wanapaswa kuwa wazalendo wa taifa.
Amesema uzalendo ni pamoja na kutumia nafasi walizopata kuihudumia jamii kwa nafasi wanazo zitumikia.
Nyihita amesema kijana kwenye nafasi ya uongozi aliyenayo aitumikie vizuri kwa kutoa huduma pasipo kupewa malalamiko.
Mjumbe huyo wa kamati ya utekelezaji ya jumuiya hiyo ya wazazi amesema kwenye uzalendo unapatikana pia uaminifu,uwajibikaji,mwadilifu,mtunza siri na muwazi.
” Ikiwa leo ni siku ya vijana kimataifa nishauri uzalendo kwa kila kijana aliye kwenye nafasi ya uongozi wa umma na uaminifu.
” Rais Dkt.Samia anawapenda vijana na anawapa nafasi za uongozi hivyo wasimuangushe na wafanye kazi kwa bidii”,amesema.
Licha ya kushauri uzalendo kwa vijana walio kwenye nafasi za uongozi wa umma ameshauri pia vijana kujiingiza kwenye masuala ya ujasiliamali ili kujiongezea kipato.
Amesema vijana wanapaswa kujifunza masuala mbalimbali yakiwemo ya ujasiliama na ulimwengu wa kidigitali kama fursa za kiuchumi.