Home Kitaifa NYIHITA AWATAKA MAAFISA TEHAMA CCM MARA KUSAJILI WANACHAMA SAHIHI

NYIHITA AWATAKA MAAFISA TEHAMA CCM MARA KUSAJILI WANACHAMA SAHIHI

Na Shomari Binda-Musoma

MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mara na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa Nyihita Nyihita amewataka maafisa Tehama wa CCM mkoa wa Mara kusajili wanachama sahihi kwenye mfumo.

Hayo ameyasema wakati akifungua mafunzo ya siku 2 kwa maafisa hao yanayofanyika kwenye ukumbi wa CCM mkoa wa Mara.

Amesema katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi oktoba mwaka huu ni muhimu kutambua na kusajili wanachama sahihi.

Nyihita amesema wanachama sahihi watasaidia kufanya kampeni na baadae kupelekea ushindi kwenye uchaguzi huo.

Amesema maafisa Tehama kutoka wilaya zote za mkoa wa.Mara wanapaswa kuzingatia mafunzo hayo na baadae kuyashusha kwenye ngazi ya chini kwa wanaofanya usajili.

“Mafunzo haya ni muhimu kwa maafisa Tehama wote katika kukisaidia Chama cha Mapinduzi kutambua na kuwajua wanachama wake”

“Tuyatumie mafunzo haya vizuri maana tukipata wanachama sahihi watatusaidia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na kupata takwimu sahihi” amesema Nyihita.

Kwa upande wake Afisa Tehama mkoa wa Mara,Paul Ngocho amesema hadi sasa wamesha sajili wanachama 115226 na wanaendelea na zoezi.

Amesema mafunzo hayo yaliyowezeshwa na Nyihita ambaye pia ni mlezi wa idara ya Tehama mkoa wa Mara itawasaidia katika utendaji wa majukumu yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!