Na Shomari Binda-Musoma
TIMU ya Nyamatare fc imekuwa ya kwanza kutinga hatua ya fainali ya mashindano ya Mathayo Cup yanayoendelea mjini Musoma baada ya kuitoa timu ya Nyakato FC
Kutangulia kwenye fainali hiyo sasa itaisubilia mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Makoko fc na Mwigobero fc itakayochezwa siku ya ijumaa.
Ilipaswa kusubiliwa mikwaju ya penati ili timu hiyo iweze kutinga fainali baada ya dakika 90 kumalizika kwa timu hizo kutoka 0-0.
Kwenye mikwaju ya penati Nyamatare imepata mikwaju 4 dhidi ya 2 ya Nyakato.
Akizungumza mara baada ya timu yake kuingia hatua ya fainali,kocha wa timu ya Nyamatare Frumence Tungaraza amesema bahati imekuwa upande wao kwenye mchezo huo.
Amesema mchezo ulikuwa mgumu na imekuwa bahati kwa upande wao kufanikiwa kuingia fainali.
Amedai mashindano ya mwaka huu yamekuwa magumu kutokana na kila timu kujiandaa vizuri kabla ya kushiriki
Amesema kwa sasa wanajipanga na mchezo wa fainali na wanaisubilia timu watakayokutana nayo kwenye hatua hiyo.
“Tunashukuru kuingia fainali na tunakwenda kujipanga ili kuchukua ubingwa we msimu huu wa mashindano ya Mathayo Cup”, amesema Frumence.