Home Michezo NYAMATARE FC NYAKATO KUCHEZA NUSU FAINALI YA KWANZA MATHAYO CUP KESHO

NYAMATARE FC NYAKATO KUCHEZA NUSU FAINALI YA KWANZA MATHAYO CUP KESHO

Na Shomari Binda-Musoma

TIMU ya Nyamatare fc na Nyakato fc kesho zitakutana kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya mashindano ya Mathayo Cup.

Mchezo huo unaosubiliwa kwa hamu na mashabiki wa soka mjini Musoma utafanyika kwenye uwanja wa shule ya sekondari Mara kuanzia saa 10 jioni

Kuelekea mchezo huo wa kutafuta timu itakayotangulia fainali tayari tambo zikitoka kwa kila timu kutamba kuibuka na ushindi.

Kocha wa timu ya Nyamatare Frumence Tungaraza amesema wachezaji wake wapo tayari kwa mchezo na ameshatoa maelekezo namna ya kuendea mchezo huo.

Amesema anatambua ugumu wa mchezo huo na kuzungumza na wachezaji wake ambao wamemuahidi kutomuangusha.

Kwa upande wa timu ya Nyskato kupitia meneja wa timu Zakayo Zakayo amesema haihofii timu ya Nyamatare na wataendeleza rekodi ya ushindi kama michezo iliyotangulia.

Amesema wachezaji wapo na ari kubwa kuelekea mchezo huo na kushukuru sapoti wanayoipata kutoka kwa mashabiki wao.

Mmoja wa waratibu wa mashindano hayo Marwa Matiku amesema maandalizi ya nusu fainali hiyo yamekamilika na kuwsomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kupata burudani

Amesema mashindano ya Mathayo Cup ni mtoko na yatakapomalizika mashindano mengine yatafuata kwa muda mfupi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!