Na Mwandishi wetu-Musoma
TIMU ya Nyakato sokoni imeipigisha kwata timu ya maafande wa FFU Mara katika mchezo wa fainali wa bonanza la mahusiano na kutwaa ubingwa.
FFU Mara wsmekubali kichapo cha bao 1-0 kwenye mchezo huo wa fainali uliofanyika kwenye uwanja wa chuo cha maendeleo ya jamii buhare na kuondoka na zawadi ya mbuzi mnyama.
Mgeni rasmi kwenye bonanza hilo mkurugenzi wa Le Grand Hotel Rama Msomi amesema amesikia changamoto za michezo Musoma mjini na kuahidi kushirikiana na wadau wengine kuhamasisha.
Akiongea kwa niaba yake,Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu manispaa ya Musoma ( FAMT) Muyenjwa Muyenjwa amesema wadau wanapaswa kujitokeza kusaidia maendeleo ya michezo Musoma mjini.
Amesema bila wadau kujitokeza kuandaa michezo mbalimbali yakiwemo mabonanza maendeleo ya michezo hayawezi kupatikana.
Mratibu wa bonanza hilo Shomari Binda amesema kama mpenda michezo ataendelea kushirikuana na kutafuta wadau mbalimbali kuandaa shughuli za kimichezo yakiwemo mabonanza.
Amesema maeneo mengine shughuli za kimichezo yakiwemo mabonanza yanafanyika mara kwa mara lakini kwa manispaa ya Musoma imekuwa changamoto
“Sisi ni watu wa michezo na tumekuwa tukiumia kuona michezo kwenye mji wetu imekuwa haina hamasa kubwa hivyo tutashiriki kuhamasisha”
“Wadau wapo kama hawa kina Rama Msomi tutawafuata watusaidie kuhamasisha shughuli za michezo kwa kuwa wana uchungu na mji huu” amesema Binda