Home Kitaifa NSSF YAZINDUA MFUMO WA KULIPIA TOZO ZA MAGARI DARAJA LA NYERERE KIGAMBONI...

NSSF YAZINDUA MFUMO WA KULIPIA TOZO ZA MAGARI DARAJA LA NYERERE KIGAMBONI KWA GHARAMA NAFUU

Na MAGRETHY GILEADY

Serikali kupitia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) imezindua Mfumo mpya ambao utasaidia kulipia gharama za magari yanayopita daraja la Nyerere lililopo Kigamboni kwa njia ya vifurushi vya bei nafuu ikiwemo kifurushi cha saa 24 , siku saba, pamoja na mwezi.

Akizungumza leo na Waandishi wa habari wakati wa ziara ya kutembelea Daraja hilo pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba wa Dungu Project Kigamboni inayotekelezwa na NSSF, Meneja Uwekezaji wa Mfuko huo Bw.Victor Luvena amesema mfumo huo unakwenda kutatua kero na kuleta ahueni kwa wananchi wanaotumia daraja hilo .

Mfumo huu unaenda kurahisisha ulipaji wa tozo za daraja kwani awali watumiaji wa daraja hili walikua wanatumia muda mwingi yaani dakika hadi 10 ,lakini kwasasa wanatumia sekunde tu kulipia ,na gharama zake ni ndogo sana ukilinganisha nazile za awali” amesema Bw. Luvena.

Naye Msimamizi wa Daraja la Nyerere Kigamboni Bw. Emmanuel Masika amesema watumiaji wa daraja hilo watalipia kifurishi cha siku kwa shilingi 2500, wiki 12000 huku cha mwezi kikiwa ni shilingi 35000 ambapo amesisitiza kuwa punguzo ya gharama hizo imeleta ahueni kwa watumiaji wa darajal la Nyerere.

Hata hivyo ziara hiyo wametembelea mradi nyumba wa Dungu nakutoa wito kwa Wananchi kuchangamkia fursa ya kupata Makazi ya kudumu kupitia mradi wa nyumba ambazo zimejengwa na Mfuko huo kwa ajili ya kupangisha na kuwauzia watu wanaohitaji kwa gharama nafuu huku wakilipia kidogokidogo ndani ya miaka 15.

Meneja umiliki wa NSSF Bw. Geoffrey Thimoth amesema kwamba mfuko huo umefanikiwa kujenga nyumba za gharama tofauti ambazo ni nyumba za kuanzia kiasi cha shilingi milioni 131, milioni 148, milioni 192, milioni 236 pamoja na milioni 497 ambapo mteja analipa asilimia 10 ya gharama ya nyumba anayoitaka halafu kiasi kingine analipa kidogokidogo kwa muda wa miaka 15.

Sisi kama NSSF jukumu letu la msingi kulipa mafao, na kuendesha miradi mbalimbali kujenga nyumba zakuzipangisha pia kuziuza kwa bei nafuu ,hivyo tuna miradi mikubwa mingi iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa na hapa tulipo ni mradi unaojulikana kama Dungu project wenye uniti mia nane za nyumba,lakini pia tuna mradi mwingine Kijichi na Tuangoma” amesema Bw. Thimoth.

Kwa upande wao Mabalozi wa NSSF akiwemo Msanii wa vichekesho Steven Mengele “Steve Nyerere”, Msanii wa Bongo fleva Willium Lymo maarufu kama “Bill Nass” pamoja Mussa Hussein wamesema Kwa nyakati tofauti wamewaasa wasanii na wananchi Kwa ujumla ambao Wana malengo ya kumiliki nyumba kuchangamkia fursa hiyo,ili kuiandaa kesho yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!