Na Boniface Gideon -TANGA
Katika kuhakikisha Wananchi wananufaika na Uchumi wa ‘Blue’ Vikundi 25 vilivyopo katika Vijiji 5 vya Halmashauri ya Mkinga mkoani Tanga vyenye zaidi ya Wanachama 750 watanufaika na mradi wa mfuko wa uhidhi Bahari (MKUBA) unaotekelezwa na Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania chini ya ufadhili wa Shirika la maendeleo la Nchini Norway ‘NORAD’.
Akizungumza leo wakati wa kukabidhi Fedha TSh.milioni 10.5 kwa vikundi 5 vya Boma kichakamiba, mratibu wa shirika la Mwambao Coastal community Network Tanzania Mkoa wa Tanga Ahmad Salim Omar amesema, Fedha hizo zitasaidia kuongeza kipato kwa Wanachama wa vyama wa vikundi 5 na kupunguza shughuli za kibinadamu zinazofanywa Baharini,
“Katika vikundi hivi 5 vya kijiji hiki cha Boma kichakamiba,jumla ya Wanachama 150 watanufaika na Fedha hizi na watajiongezea kipato cha familia zao, hii itasaidia kuongeza wigo wa fursa nyingi zaidi za kiuchumi kwa Wananchi wa kijiji hiki na kupunguza shughuli za kibinadamu zinazofanywa Baharini,na itasaidia sana kutimiza malengo ya Mradi wetu huu ambao umelenga kuongeza uzarishaji wa rasilimali Bahari na kupunguza uharibifu wa Bahari ikiwemo uvuvi Haramu unaotumia sumu ambao ni hatari kwa Afya za Viumbe wa Bahari na Binadamu” Alisisitiza Ahmed
Ahmed aliwataka Wakazi wanaoishi Mwambao wa Bahari Kutunza rasilimali za Bahari ili kuongeza uzarishaji wa Samaki,
” Niwaombe Wananchi wenzangu, mtunze rasilimali za Bahari,msikate miti hasa ya mikoko na kwa wavuvi msitumie Baruti na sumu ni hatari kwa Afya zetu walaji na Viumbe hai wa majini lakini pia tujitahidi kufanya usafi kwenye fukwe za Bahari ili tuifanye Bahari kuwa Safi muda wote, tukifanya hivyo itatusaidia kuongeza uzarishaji wa Samaki” Aliongeza Ahmad
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mkinga Octavian Moshiro aliwashukuru wadau hao wa Maendeleo kwa juhudi zao za Kutunza rasilimali za Bahari na kuwainua Wananchi kiuchumi,
” Tunawashukuru sana kwa msaada wenu na tunatambua juhudi zenu katika utunzaji wa rasilimali za Bahari na kuwainua Wananchi kiuchumi, tunaomba msichoke kutusaidia na Serikali itaendelea kuwasapatia ushirikiano ili mtimize malengo mliyojiwekea” Aliongeza
Aliwataka Wanachama wa vikundi vilivyopokea fedha hizo kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa,
” Fedha hizi mlizopokea nendeni mkazitumie kwa malengo yaliyokusudiwa,tusije tukaona mmeenda kuongeza Wanawake au kufanya sherehe na kununua sare,kafanyeni Biashara ili mjiinue kiuchumi ili familia zenu ziinuke kiuchumi na tuondokane na dimbwi la umasikini” Alisisitiza Octavian