Home Kitaifa NMB YAKABIDHI MADAWATI YA MILIONI 25 KWA SHULE TANO KIBAHA

NMB YAKABIDHI MADAWATI YA MILIONI 25 KWA SHULE TANO KIBAHA

Na Scolastica Msewa, Kibaha
Bank ya NMB imekabidhi madawati 200 na samani zingine zenye thamani ya shilingi milioni 25 kwaajili ya shule tano za msingi za Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani ikiwa ni mkakati wa Bank hiyo kurudisha fadhira kwa jamii kwa asilimia Moja ya mapato yao ya mwaka jana.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Kanda ya Pwani Dismas Prosper wakati akikabidhi madawati hayo katika Shule ya msingi Kambalage iliyopo Mailmoja Kibaha mkoani Pwani Kwaniaba ya shule zote tano za Bungo, Viziwaziwa, Kongowe, Lumumba na Kambalage.

Madawati hayo Kila Shule hizo za msingi zitapata madawati 50 huku Shule ya msingi Viziwaziwa itapata samani za Viti 16 na meza 8 za kukalia Walimu.

Msaada huo ni kati ya shilingi bilioni sita zilizotengwa na Bank hiyo kwa faida waliyopata mwaka jana ambapo hutenga asilimia Moja kurudisha kwa jamii kwa kumsaidia huduma za elimu na utunzaji wa mazingira ili jamii iendelee kufanya biashara na kuweka katika bank hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John alishukuru bank hiyo ya NMB kwa misaada ya mara kwa mara katika kuhudumia Wananchi wa Wilaya ya Kibaha.

Amesema katika Utawala wa awamu ya sita imefanya juhudi kubwa ya kujenga shule mpya mbili za msingi na shule mpya mbili za Sekondari wilayani humo ikiwa ni pamoja na kuajiri Walimu wapya 900 sambamba na kupandisha madaraja Walimu 190.

Amefafanua kuwa kuhusu suala la elimu serikali peke yake haitoshi kushughulikia bila Wadau wengine kushiriki hivyo alishukuru bank ya NMB kwa msaada huo wa madawati.

Diwani wa Kata ya Tumbi Raymond Chokala ameshukuru kwa msaada huo na kuwaomba tena bank hiyo kuendelea kutoa msaada shuleni hapo kwani bado Kuna upungufu wa madawati 53.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Kambarage Happiness Msaki alisema msaada huo wa madawati umesaidia kuweka utulivu kwa Wanafunzi darasani tofauti na awali kabla ya kuletwa madawati hayo kwani hata asubuhi walikuwa wakiingia madarasani kwa utulivu bila kusukumana kwa lengo la Kila mmoja kutaka kuwahi pakukaa.
++++++++

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!