Na Yusuph Mussa, Mbeya
BENKI ya NMB imepanga kusomesha elimu ya juu kwa watoto wanaotoka kwenye kaya zenye mazingira magumu ikiwemo wenye kipato duni. Nia ikiwa kuwasaidia watoto wa makundi hayo kupata elimu.
Hayo yalisemwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Ruth Zaipuna kwenye Mkutano Mkuu wa 36 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaofanyika jijini Mbeya kwa siku tatu, ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango.
“Benki imeanzisha asasi maalum ya kiraia ya NMB Foundation itakayosaidia kwenye sekta za elimu, afya, ujasiriamali na mazingira. Asasi hii ilizinduliwa mwaka jana na tayari kwa mwaka huu wanafunzi 100 watapata ufadhili wa masomo ya elimu ya juu, ambapo benki itawalipia ada, malazi, fedha ya kujikimu, nauli ya kwenda chuo na ya kurudi nyumbani pamoja na kuwapatia kompyuta mpakato kwa ajili ya kuwasaidia katika masomo yao kupitia Nuru Yangu Scholarship” alisema Zaipuni.
Zaipuni alisema, kama kauli mbiu