Na Elizabeth John,Njombe.
Benki ya NMB imekuja na mpango wa kufadhili masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi 100 wanaotoka mazingira magumu ambao wanafanya vizuri katika masomo yao ikiwa ni njia moja wapo za kusaidia jamii.
Hayo yamesemwa na mkuu wa idara ya huduma na biashara za serikali NMB Vicky Bishubo,katika uzinduzi wa Mwalimu Spesho iliyofanyika mjini hapa.
Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka,amesema uwepo wa Mwalimu Spesho kupitia benki ya Nmb utasaidia janga la walimu kutapeliwa mara kwa mara na watu au taasisi zenye riba kubwa.