Shilingi tilioni 1.61 zimetolewa mikopo ndani ya miaka sita katika benki ya NMB kwa kuwezesha ufugaji wa samaki na mazao ya chakula nchini
Akitoa taarifa wakati wa ufunguzi wa Maonyesho Jumuhia ya Wafugaji kibiashara nchini TCCS Mkuu wa Idara ya Ushauri wa Kilimo Isaac Masusu huko Ubena Chalinze mkoani Pwani amesema pia bank hiyo imetoa mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni 20 ambazo zimeelekezwa katika program ya kujenga kesho iliyobora BBT.
Masusu amesema NMB inatambua changamoto ya upungufu wa mitaji ambayo hupunguza uzalishaji wa kisasa wenye tija na ndio maana wamefanya kuwezeshaji huo wa mikopo.
Amefafanua kuwa benki ya NMB imekuwa ndio benki ya kwanza nchini kuanza kutoa mikopo ya riba nafuu na tulitoa zaidi ya bilioni 100 kwa wakati huo na pesa hiyo ilitolewa kwa Wafugaji nchini.
“Lakini pia benki yetu inatoa mafunzo kwa wakulima kupitia taasisi tatu za NMB foundation, mafunzo hayo ni kwa vijana na akina mama pamoja na wafugaji kwenye maeneo yao pasipo gharama yoyote” alisema Masusu
Awali Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafugaji wa Kisasa Tanzania NCCS ,Naweed Mulla amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan kutikana na serikali kuwashika mkono wafugaji wa kisasa.
Mulla amesema kuwa maonesho haya yanalenga kuwanyanyua wananchi na wafugaji wa kisasa pamoja na kuwawekea mazingira sahihi huku amesema kuwa kauli mbiu ya mwaka huu inasema tufuge kibiashara tuijenge kesho iliyo bora.
“Mhe.Rais amekua akitupa maneno ya kututia moyo pindi awapo katika majukwaa mbalimbali jambo ambalo linazidi kutuje nga na kutukuza zaidi” amesema Naweed.
Mwenyekiti huyo wa TCCS Naweed amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amewapa bajeti mara mbili kwa kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi hivyo tunaahidi kutoa ushirikiano wa kutoa maoni yetu katika sekta hii ya ufugaji wa kisasa na tuna ahidi tutakuwa naye bega kwa bega katika kukuza uchumi wa nchi kupitia ufugaji wa kisasa.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti akifungua Maonyesho hayo aliwapongeza Jumuhia ya Wafugaji kibiashara kwa kufanya Maonyesho hayo yanayoonyesha Uhalisia wa ufugaji wa kibiashara ambao utasaidia kuongea Soko la nyama ya Tanzania Kimataifa.
Tanzania ni nchi ya pili kwa mifugo barani Afrika pia tuna ng’ombe zaidi ya Mil.37.
Maonesho hayo yamefunguliwa jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Alexander Mnyeti yafungwa kesho ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri Mkuu Biteko.