Home Kitaifa NIRC-SHERIA INAMSAIDIA MKULIMA KUONDOA CHANGAMOTO

NIRC-SHERIA INAMSAIDIA MKULIMA KUONDOA CHANGAMOTO

Na Monica sibanda -Dodoma

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji(NIRC) imesema sheria ya umwagiliaji imetungwa ili kuondoa changamoto zilizokuwa zinazoikabili sekta ya umwagiliaji nchini.

Akizungumza leo Agosti 5,2024 kwenye maonesho ya Kimataifa ya wakulima yanayoendelea kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma Afisa Sheria mwandamizi NIRC Amina Mweta amesema ushiriki mdogo wa wakulima na sekta binafsi katika kuendeleza kilimo cha umwagiliaji ni chanzo cha uanzishwaji wa sheria hiyo.

“Sheria ya Taifa ya umwagiliaji na.4 ya mwaka 2013 imetugwa na kupitishwa na bunge mwaka 2013 ikatiwa saini na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan octaba 20,2013 sheria hii imeanzishwa na tume ya umwagiliaji ili kusimamia kilimo cha umwagiliaji na kutatua changamoto za wakulima”,Amesema.

Ameongeza kuwa sababu nyingine ya kuanzishwa sheria hiyo ni pamoja udhaifu wa mifumo ya kitaasisi ambao ulikua haukidhi kasi ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji lakini pia uvamizi wa maeneo ya ardhi yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji.

Sambamba na hayo amebainisha vitendo vilivyokatazwa katika sheria ambapo ni pamoja na kuingia katika ardhi ya umwagiliaji kwa madhumini tofauti na umwagiliaji.

Lakini pia,kuruhusu sumu ya viwandani au uchafu wa majumbani kuingia kwenye skimu yeyote ya umwagiliaji bila kutibu maji kikamilifu

Aidha amesema kutokana na hali iliyokuwepo na changamoto ambazo zimeikabili sekta ya umwagiliaji sheria imesaidia kuongezeka kwa mchango wa umwagiliaji katika uzalishaji wa chakula na lishe lakini pia kuongezeka kwa pato la wakulima na Taifa kwa ujumla.

Naye Mhandisi Mwandamizi wa Umwagiliaji Mha.Naomi Mcharo amesema kwa mwaka huu wa fedha NIRC wamejipanga kuchimba visima 1000 nchi nzima.

Aidha amesema NIRC wanaendelea na miradi mbalimbali ya umwagiliaji nchini ili kuhakikisha kilimo cha umwagiliaji kinakuwa na kumnufaisha mkulima.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!