Home Kitaifa NIC YAWATAKA WANAHABARI KUKATA BIMA YA PERSONAL ACCIDENT

NIC YAWATAKA WANAHABARI KUKATA BIMA YA PERSONAL ACCIDENT

Waandishi wa habari wametakiwa kukata bima ya Personal Accident ili iweze kuwalinda wanapokuwa kazini au nje ya kazi.

Hayo yamesemwa na meneja wa shirika la bima kanda ya ziwa (NIC) Stela Mrwa wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofika katika ofisi hizo ili kujua shunghuli mbalimbali zinazofanywa na NIC pamoja na kuzungumzia Usiku wa wadau wa habari kanda ya ziwa utakaofanyika tarehe 20/10/2023.

Stela amesema bima ya Personal Accident ni muhimu kwa wanahabari kwa kuwa mwanahabari anaweza kupata ajali akiwa kazini au anaweza kupata ajali akiwa nyumbani kutokana asili ya kazi yake.

Bila shaka mmewahi kusikia mwandishi wa habari amevamiwa na kujeruhiwa akiwa kazini au nyumbani sasa bima hii ya Personal Accident itamfidia mwanahabari huyu endapo atapata majanga hayo”.alisema Stela

Kwa upande wa wananchi Stela amewataka kukata bima za nyumba ili waweze kulinda nyumba zao na mvua na majanga ya asili ambayo yanaweza kujitokeza.

Stela amesema ni vema wananchi wanaomiliki nyumba wakakata bima za nyumba ili waweze kujikinga majanga yasiyoweza kuzuilika kama vile mafuriko au ajali ya moto ili majanga hayo yakitokea waweze kulipwa fidia kupitia bima za nyumba.

Wote tunasikia kupitia vyombo vya habari kuwa kuna mvua kubwa zitanyesha hapa nchini sasa niwashauri wananchi mkate bima ya nyumba hii italinda nyumba na majanga kwa hiyo niwaombe wananchi tusipuuze wataalamu wa utabiri wa hali ya hewa maana wamesema kuna hizo mvua kubwa na zinaweza kuleta madhara sisi NIC tupo tayari kuwalipa fidia”.alisema Stela

Akizungumzia usiku wa Wadau wa Habari Kanda ya Ziwa,Stela amekipongeza chama cha waandishi wa habari mkoa (MPC) kwa kuandaa usiku huo utakaowakutanisha wadau wa habari kwa lengo la kufahamiana na kubadilishana mawazo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!