Na Dickson Mnzava, Same.
Mbunge wa Jimbo la Same mashariki Mkoani Kilimanjaro mheshimiwa Anne kilango Malecela ametoa shukrani zake kwa serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwanamna ambavyo serikali yake imeweza kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye Jimbo hilo.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya msaragambo wa pamoja na wananchi kwenye eneo ambalo linajengwa Shule hiyo ya sekondari na ufundi (AMALI) mradi unaotekelezwa na wahandisi wa halmashauri ya Wilaya ya Same katika Kata ya Kihurio mheshimiwa Anne kilango amesema katika kipindi chake chote cha ubunge hajawi kupata miradi mingi ya maendeleo kama kipindi hiki.
Amesema kukamilika kwa mradi huo mkubwa wa Shule hiyo ambao kwasasa umetengewa kiasi cha milioni 584 utakuwa mkombozi kwa wananchi wa Wilaya ya Same na Mkoani Kilimanjaro kwaujumla kwani shule hizo ni chache mno kwenye Mkoa huo ambao Same ni Wilaya ya tatu kuwa na shule hiyo kimkoa.
“Ndugu zangu katika siku ambayo nimefurahi kupitiliza ni pamoja na leo hakika kipekee nimshukuru sana Mheshimiwa Rais Mama Samai kweli ametujali sana wana Same mashariki ukweli kupata mradi huu kwetu sasa kama wananchi ni fursa kubwa ya maendeleo Katika Jimbo letu hivyo niwapongeze wananchi wangu kwa kuupokea mradi na asitokee yeyote wa kuturudisha nyuma sisi ni mbele kwa mbele”
“Alisema Mama Anne kilango”
Kwaupande wake mtaalam Kutoka ofisi ya mhandisi wa ujenzi toka halmashauri ya Wilaya ya Same Margareth Mkenda amesema kwasasa jumla ya majengo ya utawala,madarasa mawili,maabara ya biolojia na fizikia pamoja maktaba yataanza kujengwa huku akisema watahakikisha kila hatua ya kitaalam kwenye ujenzi wa Shule hiyo utafuatwa kabla ya kuanza majengo hayo ili kuweza kuepusha changamoto ndogo ndogo.
Diwani wa Kata ya Kihurio Mariane Mariane na wananchi wa Kata hiyo akiwemo Selemani Seif wao wameipongeza serikali na mbunge wao Anne kilango kwa kutoa fedha hizo huku wakisema uwepo wa shule hiyo sasa utakuwa muarobaini wa changamoto ya ajira kwa vijana walio wengi kwani sasa vijana watakuwa wakipata ujuzi mbalimbali kupitia shule hiyo na wanapomaliza shule wanaweza kujiajiri katika fani mbalimbali walizojifunza.
Mradi huo wa Shule ya sekondari ufundi (AMALI) majengo yake yameanza kupimwa kwaajili ya kuanza ujenzi huo kwenye Kata ya Kihurio huku mbunge wa Jimbo hilo la Same mashariki Anne kilango Malecela akiwahimiza wananchi kujitoa kwa wingi kwaajili ya mradi huo ambao utachukua ukubwa wa eneo la ekari 56 na ukiwa unatekelezwa katika Kijiji cha Azambara Kata ya Kihurio.