Home Afya NHIF YABORESHA KITITA CHAKE CHA MAFAO

NHIF YABORESHA KITITA CHAKE CHA MAFAO

Mkurugenzi Mkuu  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya  (NHIF),  Bernard Konga, akizungumza alipokuwa akiwasilisha mafanikio ya mfuko huo katika miaka mitatu ya serikali ya Awamu ya Sita, katika mkutano wa Wahariri na waandishi wa Habari uliofanyika leo Machi 7,2024 Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina, Thobias Makoba, akizungumza alipokuwa akitoa neno la utangulizi mapema kabla ya Mkurugenzi Mkuu wa NHIF kutoa wasilisho lake katika Mkutano huo.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Anitha Mendoza, akiwa pamoja na Wahariri wengine katika mkutano huo.

Mjumbe wa Kamati Tendaji TEF, Salim Said Salim akizungumza alipokuwa akitoa neno la shukrani mapema kabla ya kuhitimishwa kwa mkutano huo.

(PICHA NA HUGHES DUGILO)

DAR ES SALAAM 

Mkurugenzi Mkuu wa  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bernard Konga, amesema kuwa Maboresho yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ya Mheshimwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Afya, umewezesha Mfuko huo  kupata mafanikio makubwa  na kwamba mfuko huo umeendelea kuboresha kitita chake na kutoa kitita cha mafao chenye wigo mpana ukilinganisha na skimu zingine za Bima ya afya.

Konga amebainisha hayo alipokuwa akiwasilisha mada katika mkutano wa Wahariri na waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya mfuko huo katika kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema ndani ya miaka mitatu ya Uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kumekuwa na Mabadiliko kwenye Ugharamiaji wa Huduma za Kibingwa na Bobezi.

“Gharama za Kugharamia Wagonjwa wa Saratani kwa mwaka 2023/2023 zilikuwa Shilingi Bilioni 32.46, ukilinganisha na Bilioni 12.25 mwaka 2021/2022, huku kwa Upande wa maradhi ya Figo ikiwa Shilingi Bilioni 35.40 na Bilioni 11.45” amesema Konga.

Kuhusu mpango wa Bima ya Afya kwa Wote, Konga amesema Chimbuko lake ni kutimiza wajibu wa Serikali Kikatiba kuhakikisha Wananchi wanakua na uhakika wa kupata huduma bora za Afya bila Vikwazo.

“Uhalisia unaonesha kuwa asilimia 85 ya Wananchi hawana Bima ya Afya na hivyo kukosa uhakika wa Huduma Bora za Afya kipindi wanahitaji” ameeleza Konga.

Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya utendaji kutoka jukwaa la wahariri Tanzania (TEF),  Said Salim Said aliwapongeza NHIF kwa kutekeleza wajibu wao kwa kuendelea kuelimisha umma namna ambavyo wanafanya kazi zao kwa ufanisi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!