Home Kitaifa NEMC WAKIADHIMISHA SIKU YA MASHUJAA KWA KUSHIRIKI USAFI HOSPITALI YA WILAYA YA...

NEMC WAKIADHIMISHA SIKU YA MASHUJAA KWA KUSHIRIKI USAFI HOSPITALI YA WILAYA YA MAFIA

Wafanyakazi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Kanda ya mashariki kusini wameadhimisha siku ya mashujaa kwa kushiriki kufanya usafi katika mazingira yanayozunguka Hospitali ya wilaya ya Mafia mkoani Pwani.

Maadhimisho hayo yamefanyika kwa ushirikiano wa Viongozi, Wafanyakazi wa Halmshauri ya wilaya ya Mafia na baadhi ya Wananchi waliofika hospitalini hapo kutoa ushirikiano wa usafi huku wananchi wengine wakiendelea na usafi katika makazi yao na maeneo ya biashara wilaya nzima ya Mafia.

Akiongoza Wafanyakazi wa NEMC Kanda ya mashariki kusini Afisa Mwandamizi wa NEMC Gift Ngowo katika kufanya usafi huo wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa amezitaka halmashauri nchini kuzingatia usafi katika Hospitali zao kwa kujenga kichoma taka na kuzisimamia taka za hospitali.

“Mfano mzuri ni hapa Hospitali ya wilaya ya Mafia Wana kizimba cha kuchomea taka na Wana utaratibu kutenganisha taka zinazozalishwa katika shughuli za kitabibu hivyo tunasisitiza na wengine waige mfano huu wa kusimamia vizuri suala zima la usafi na utunzaji wa mazingira” alisema Ngowo.

Ngowo amesema Katika Hospitali hiyo ya wilaya wameshiriki kufanya usafi huo na kukagua na kuangalia mazingira yanayozunguka Hospitali hiyo na kushauri kuhusu utunzaji wa mazingira.

Amesema ushujaa unaanza katika usafi wa mazingira ili kila mtu afanye shughuli zake kwa usalama mwenye afya njema na ndio maana wameshiriki kufanya usafi huo.

Awali Katibu tawala wa Wilaya ya Mafia Olivanus Thomas alisisitiza suala la uzalendo kwa Watumishi wa serikali wa wilaya hiyo katika kuwahudumia Wananchi.

“Kwenye shughuli zetu za kila siku tuendelee kuwa Wazalendo kama ni kulipa Kodi lipa Kodi, kama nikukusanya Kodi kusanya Kodi na kama ni kutoa huduma toa huduma nzuri ili uweze kuwa shujaa wa kesho” alisema Thomas.

“Hakuna shujaa leo hii tunamkumbuka ambaye hakuwa Mzalendo hivyo uzalendo wetu wa leo ndio utatengeneza ushujaa wa kesho “ alisema Thomas

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!