Home Kitaifa NDARUKE AITAKA TARURA KIBITI KUPITIA UPYA MIKATABA NA WAKANDARASI

NDARUKE AITAKA TARURA KIBITI KUPITIA UPYA MIKATABA NA WAKANDARASI

Kamati ya siasa ya CCM Wilaya ya Kibiti imetoa siku 9 kwa Wakala wa Barabara vijijini (TARURA) Wilaya ya Kibiti kurekebisha Barabara ya changarawe ya Bungu kwenda Kijiji cha Mchungu, ambayo serikali imekwishalipa zaidi ya shilingi milioni 300.

Akitoa maelekezo baada ya ukaguzi wa utekelezaji wa ilani ya CCM Wilaya ya Kibiti, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibiti, Juma Ndaruke, ameitaka TARURA Wilaya ya Kibiti kupitia upya mikataba waliyoingia na wakandarasi kujenga barabara wilayani humo ili wajiridhishe kama kilichotekelezwa kinaendana na kiasi cha fedha ambacho serikali imelipa sambamba na kuangalia ubora wa barabara hizo.

Amesema, “TARURA wapitie upya kuhakiki ubora wa utekelezaji wa miradi ya barabara wilayani humo ili utekelezaji wa miradi uendane na thamani ya fedha za serikali zilizolipwa.”

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Kanali Joseph Kolombo, amesema barabara vijijini hutengenezwa kwa ajili ya kurahisisha huduma za usafiri ikiwemo usafirishaji wa mazao yao kwa urahisi.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Kibiti, Eng. Ayubu Ngereza, amesema changamoto ya barabara hiyo inatokana na mvua nyingi zilizonyesha wilayani humo na ameahidi kuifanyia ukarabati haraka kama walivyoagizwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!