Home Kitaifa TANZANIA YAOMBWA KUCHANGIA MFUKO WA GLOBAL FUND

TANZANIA YAOMBWA KUCHANGIA MFUKO WA GLOBAL FUND

Na Magreth Mbinga

Kila mwaka kuna vifo zaidi ya elfu sabini na mbili ambavyo vinasababishwa na ugonjwa wa Maralia mfuko wa Global fund unatoa pesa za kupambana na vifo hivyo katika Nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Global fund hapa Nchini Dk Peter Bujai na kusema kuwa mfuko huo umesaidia sana katika kudhibiti magonjwa ya maralia ,virusi vya ukimwi na kifua kikuu.

“Septemba 19 mpaka 21 mwaka huu Nchini Marekani katika Jiji la New York kutafanyika uchangiaji wa pesa kwa awamu ya saba kwaajili ya mfuko wa Global fund ili kuendeleza kazi ambayo imeanza kufanyika kwa miaka mingi”amesema Dk Bujai.

Pia amesema katika uchangiaji huo Nchi zinazoendelea wanaahidi kiasi cha pesa ambazo zitatoa na kwa mfuko wa Global fund umekadiria kuanzia mwaka 2022-2026 unahitaji Dola za Kimarekani Bilioni 18 ambapo kunakuwa na makundi mawili kutoka Nchi zinazoendelea na Nchi zilizoendelea.

“Toka mwaka 2002 Nchi ya Tanzania imefaidika na mfuko huo kwa kiasi cha Dola za Marekani Bilioni 2.6 katika miradi ambayo mfuko umeichangia na katika pesa hizo ambazo Nchi imepokea karibu watu Milionj 1.2 wapo kwenye dawa za kufubaza virusi vya ukimwi na zaidi ya watu Milioni 8.2 wamepata kutibiwa maralia na karibu watu elfu 84 wametibiwa na kupona kifua kikuu”amesema Dk Bujai.

Aidha amesema Nchi za Afrika zimechangia mfuko mfano Afrika ya kuaini,Kenya,Benin,Namibia,Lesotho,Cordva,Togo na Zimbabwe zimechangia mfuko wa kifua kikuu katika miaka tofauti .

“Nchi yetu ionyeshe mshikamano na Nchi zingine kama wengine wameweza kuchangia sisi tunazidi kubaki nyuma pamoja na vipaumbele vyetu ambavyo tunavyo hili ni jambo la muhimu sana kwa Nchi yetu tunaiomba Serikali yetu kulichuku hili “amesema Dk Bujai

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!