Home Kitaifa NCAA YAALIKA WANAWAKE KUTALII NGORONGORO KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

NCAA YAALIKA WANAWAKE KUTALII NGORONGORO KUELEKEA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

Kassim Nyaki, Arusha.

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani tarehe 8 machi, 2025 Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa kushirikiana na kampuni ya Tanzania Coorporates imeandaa safari ya siku moja kwa wanawake kutembeela vivutio vya utalii vilivyopo katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro.

Akitangaza kampeni hiyo jijini Arusha Kamishna msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi anayesimamia idara ya huduma za Utalii na Masoko ameeleza kuwa Safari hiyo ya siku moja (Day Trip) itafanyika tarehe 7 Machi, 2025 kuanzia Jijini Arusha ambapo ina lengo la kuunganisha wanawake katika sekta ya utalii ili kuunga mkono jitihada za serikali katika kutangaza Utalii wa ndani kwa kutembelea Kreta ya Ngorongoro.

“Kama mnavyojua Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara namba moja kutangaza Utalii wa vivutio tulivyokuwa navyo hapa nchini, mtakumbuka Filamu ya Tanzania the Royal Tour na Amaizing Tanzania yeye ndio amekuwa Jasiri muongoza njia kutangaza utalii wa nchi yetu duniani, kwa kuelekea siku hii tumeamua kuungana na kuhamasisha wanawake kufanya utalii wa ndani katika eneo la hifadhi ya Ngorongoro.

Mkurugenzi wa Tanzania Coorporates Elina Mwangomo ameeleza kuwa gharama ya safari hiyo itakuwa shilingi 170,000 pekee kwa kila mtu ambapo gharama hiyo itajumuisha kiingilio, chai ya asubuhi, chakula cha mchana, usafiri, gharama za muongoza watalii pamoja na kila mshiriki kupewa kofia atakayovaa wakati wa safari ya Utalii.

“Sisi kama wanawake wa Sekta ya Utalii tumeamua kumuunga mkono Kama mnavyojua Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara namba moja kutangaza Utalii wa vivutio tulivyokuwa navyo hapa nchini, mtakumbuka Filamu ya Tanzania the Royal Tour na Amaizing Tanzania yeye ndio amekuwa Jasiri muongoza njia kutangaza utalii wa nchi yetu duniani.

kwa kuhamasisha wanawake wajitokeze kwa wingi kuungana katika safari hii ya kufanya Utalii Ngorongoro ambapo tunaamini wote watakaolipia kifurushi cha 170,000 kwenda kutalii Ngorongoro watapata uzoefu mzuri usiosahaulika katika Maisha yao (unforgettable experience) na watarajie kuona mtawanyiko wa wanyama mbalimbali ikiwemo Wanyama wakubwa watano ambao ni Simba, chui, Faru, tembo na Nyati wakiwa katika mazingira ya asili na katika safari hii watapata huduma ya usafiri uliopo katika kiwango kizuri na usalama wa kutosha wakati wote wa safari.

Kwa upande wake mwakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Thabea Mollel amewahakikishia wanawake wote watakaoshiriki safari ya utalii Ngorongoro watapata usalama wa hali juu katika safari ya utalii katika hifadhi ya Ngorongoro na kurudi Arusha.

Wanawake ambao watahamasika kuunga mkono jitihada za utalii wa ndani wanaweza kupiga namba 0758171914 au Namba 0763 291179 kisha watapewa utaratibu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!