Home Kitaifa NBC BENKI YAJA NA KAMPENI KABAMBE KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI ZA KIFEDHA

NBC BENKI YAJA NA KAMPENI KABAMBE KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI ZA KIFEDHA

Na Magrethy Katengu

Benki ya bishara ya NBC imekuja na fursa ya kuhakikisha wananchi wananufaika kwa kutumia huduma mbalimbali ikiwemo wafanyabishara, wakulima, wafanyakazi serikali binafsi kwa kutoa elimu ya kifedha ili Waweze kukuza uchumi wao kupitia benki hiyo

Akizungumza Leo Jijini Dar es salaam Mkuu wa Masoko wa Benki ya NBC David Rymond Wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya “SHINDA MECHI ZAKO” ambapo amesema kampeni hiyo imeshirikisha wadau mbalimbali ikiwemo wadau wa soka wachambuzi Bodabona watazunguka kila mtaa kwa kuwafunguli Wananchi akaunti za benki na itaendeshwa kwa kutoa elimu ya Kifedha

Jina la Kampeni shinda Mechi zako Lina na Maana kuwa timiza malengo yako kupitia benki ya NBC kwa kufungua akaunti kuwa familia na kupata huduma za mikopo kwa riba nafuu, kuweka fedha zako katika benki hiyo kwani kuna hadi akaunti ya timiza malengo yako ukifurahia popote ulipo ” amesema Mkuu wa Masoko

Hata hivyo NBC ni Wadhamini wa Soka nchini hivyo tunatoa elimu kwa muda wa miezi 3 kutatua changamoto za kijamii hlikiwemo Ada za wanafunzi mitaji ya biashara hivyo Wapo tayari kupitia Kampeni hiyo wananchi wanakwenda kutatuliwa changamoto zao za kifedha

Naye Abedi Kasebo Mkuu wa bidhaa na mauzo benki ya NBC amesema wamekuja na bidhaa ya mikopo ya riba nafuu na akanti maalumu za Watoto,malengo,mishahara, na malengo na huduma nyingine za ATM card hivyo wateja wanahudumiwa popote walipo katima mitaa NBC wahudumu watakapopita wasisite kuwaita na kuuliza .

Naye Mchambuzi wa Michezo Shafii Dauda ameshukuru benki hiyo kwa kuwa wadau muhimu kudhamini soka la ndani hivyo hata vilabu vya mpira vyote vinatambua mchango huo mkubwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!