Na Shomari Binda-Musoma
MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amesema anataka Musoma iwe ya kufanya kazi,mazoezi na michezo na kupata burudani ya starehe.
Kauli hiyo ameitoa leo oktoba 5 kwenye bonanza kubwa la michezo mbalimbali lililofanyika kwenye uwanja wa Posta.
Amesema anataka kuiona Musoma iliyochangamka kwa watu wake kufanya kazi kwa bidii awe mtumishi wa umma au binafsi na baadae kushiriki mazoezi ,michezo na starehe” kula bata”.
Chikoka amesema bila kuwa na afya njema mtu awezi kufanya kazi na kushiriki mazoezi na michezo kunafanya mwili kuchangamka.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imempendeza kumleta Musoma na anataka Wilaya ichangamke kwa kufanya kazi,mazoezi na matukio ya kimichezo ya mara kwa mara.
” Leo tumekutana kwenye bonanza letu hili ikiwa ni katika kuweka mwili sawa na hii sio mwisho bali itakuwa endelevu.
” Nimeshukuru kuona Kata zote 16 wakiwemo wanawake,wanaume kwa vijana wamejitokeza kushiriki bonanza hili na nimefarijika”,amesema.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi walioshiriki bonanza hilo wamemshukuru mkuu huyo wa Wilaya kwa kuanzisha utaratibu wa kufanya mazoezi.
Mmoja wa washiriki hao Adam Chiguma amesema wazo la mkuu wa Wilaya linapaswa kuungwa mkono na kila mmoja kwa kuwa ni jambo jema.
Kabla ya kufanyika michezo mingine bonanza lilianza na jogging mapema asubuhi na kwenye mchezo wa soka timu ya Biashara United veteran waliibuka mabingwa kwa kuifunga Musoma veteran bao 1-0 huku mchezo wa netball timu ya Kamnyonge wamekuwa washindi kwa kuwafunga Mwisenge 15-7 na mchezo wa rede washindi wamekuwa Kamnyonge