Na Magrethy Katenga
Bodi ya Baraza la Ujenzi(NCC) imetakiwa kuhakikisha inatekeleza masuala muhimu yatakayoendesha shughuli zao ikiwemo kutunga sheria ya majenzi hiyo kutunga sheria ya majenzi,kuja na miongozo ya ujenzi, kanuni za ujenzi na kuifanya tasnia ya ujenzi iheshimike
Aliyasema hayo Jijini Dar es salaam Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi-Sekta Uchukuzi Atupele Mwakibete katika hafla ya uzinduzi wa bodi bodi mpya ya baraza hilo NCC ambapo amesema kilio kikubwa cha serikali ni miradi yake kuwa na gharama kubwa ambayo imetokana na kukosa miongozo sahihi wa ujenzi.
“Niitake bodi ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) hii mpya kutoa miongozo ya thamani halisi ya miundombinu ya Barabara ili kuokoa pesa za serikali zinazopotea kutokana na kukosa miongozo hivyo tungenisheria ya majenzi, miongozo ya ujenzi, kanuni za ujenzi kuifanya tathnia ya ujenzi iheshimike”alisema Naibu Waziri
Hata hivyo ameikata Bodi hiyo kuhakikisha wanazingatia sheria za utumishi wa umma na kuacha kufanya vitendo vya udanganyifu ikiwemo vya rushwa bali wawe mfano katika kutekeleza miradi mbalimbali kwani wameaminiwa ndani ya miaka mitatu kiwepo na Mabadiliko makubwa.
Naibu Waziri Mwakibete amewakumbusha kuwa matarajio ya serikali ni pamoja na kupata mabadiliko makubwa katika taasisi hiyo kwa mafanikio makubwa kwa mujibu wa mipango ya kila mwaka.
‘Nakuagiza Naibu Katibu Mkuu ujenzi kwa niaba ya Katibu Mkuu mabadiliko haya watakayokuwa wanaleta kwenu muweze kuyasimamia,kuyaratibu na kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo ili lengo lililokusudiwa litimie ’alisema Naibu Waziri Mwakibete
Awali akitoa taarifa kuhusiana na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC),Afisa Mtendaji Mkuu wa baraza hilo Dkt Matiko Mturi ameyataja majukumu yake kuwa ni pamoja na kuwezesha maendeleo ya kukua kwa sekta ya ujenzi nchini.
Dkt Mturi ameeleza kuwa jukumu lingine ni kufanya utafiti na kuratibu kufanyika kwa utafiti utakawezesha maendeleo katika sekta ya ujenzi lakini pia kuwezesha migogoro inayotokea katika sekta ya ujenzi hasa kwenye miradi ya ujenzi kupata utatuzi wa haraka na kuleta tija.
‘Pamoja na kuwa na mafanikio tumekuwa na changamoto chache ikiwemo ya uhaba wa wataalamu wa kada za uhandisi,za ukadiriaji majenzi na kada za ubunifu majengo hivyo tunaiomba serikali iliangalie hili kwa jicho la tatu
Naye Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Dkt Fatma Mohamed ameshukuru kwa kuaminiwa kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitatu hivyo ameahidi kuwa watafanya kazi kwa bidii na weledi kwa kutekeleza maagizo yote waliyopatiwa na kutimiza majukumu yao ipasavyo ili kuleta mabadiliko katika sekta ya ujenzi nchini.