Home Kitaifa NAIBU WAZIRI TAMISEMI ATOA SIKU 15 TARIME UJENZI VYUMBA VYA MADARASA KUKAMILIKA.

NAIBU WAZIRI TAMISEMI ATOA SIKU 15 TARIME UJENZI VYUMBA VYA MADARASA KUKAMILIKA.

Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEM David Silinde amempa siku 15 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoa wa Mara kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa baada ya halmashauri hiyo kua nyuma katika utekelezaji wa ujenzi huo kuliko halmashauri mwenzake ya Tarime Vijijini ambao wapo katika hatua nzuri ya ukamilishaji wa madaraa hayo katika shule za sekondari.

Hayo ameyasema akifanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa Vyumba vya madarasa hayo katika Mkoa wa Mara kwa siku ya pili na kubaini kua halmashauri ya mji wa Tarime bado wapo nyuma sana na kutaka mpaka ifikapo terehe 15 ya mwezi ujao awe ametumiwa taarifa ya ukamilishaji wa madarasa hayo yakiambatana na picha na atarudi mwenyewe kukagua kwani inaonesha kuna uzembe umefanyika mpaka sasa kua nyuma katika ukamilishaji.

“Nimetoka Tarime vijijini wao wapo wanamalizia katika ukamilishaji wa madarasa hayo katika kupiga rangi na wengine washamaliza na vifaa vyote wananunua hapa mjini kwanini nyinyi mpaka sasa bado, mkurugenzi nataka taarifa baada ya siku 15 kuona mlivyokamilisha na picha ofisini kwangu kama mlivyohaidi kua siku hizo mtakua mmekamilisha ujenzi na nitarudi kukagua” Silinde

Kwa upande wake Mbunge wa Tarime vijijini Mwita Waitara amemuomba Naibu Waziri Silinde waweze kupatiwa mabweni katika shule yao ya sekondari Kemambo kwani kwasasa wanakabiliwa na tatizo la baadhi ya wanafunzi kua watoro na kukimbilia kwenda kufanya kazi migodini ili wapate fedha.

Kwa upande wake Naibu Waziri amesema serikali imelichukua jambo hilo na wapo mbioni kutoa fedha za ujenzi wa mabweni hasa katika shule ambazo zipo mbali ana zile zilizopo katika jamii za kifugaji ili kuwafanya wanafunzi wasome kwa utulivu bila kuingiliana na shughuli za kijamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!