Home Kitaifa NAIBU WAZIRI MKUU DOTO BITEKO ATOA MAELEKEZO EWURA KUHUSU BEI YA MAFUTA...

NAIBU WAZIRI MKUU DOTO BITEKO ATOA MAELEKEZO EWURA KUHUSU BEI YA MAFUTA KUPANDA

Na Magrethy Katengu

Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti huduma za Nishati na MajinEWURA imesema itahakikisha inashughulikia kwa haraka changamoto zinazopelekea uhaba wa mafuta nchini unahimilika kwa kupitia mfumo mzima wa upangaji wa bei ili kusaidia wananchi kuwapunguzia kiwango cha ukali wa gharama za kupanda bei za bidhaa

Ameyasema halo leo Naibu Waziri Mkuu ambye pia ni Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko katika kikao kazi na Watumishi wa EWURA Kanda ya Dar es salaam alipofanya ziara yake ya kutembelea ofisini hapo ambapo amesema sasa kunaachangamoto ya mafuta nchini na sio Tanzania pekee ni duniani lakini pamoja na changamoto ziko sababu ambazo ni nje ya Tanzania mfano ukosefu wa dola, uzalishaji wamafuta, gharama kubwa za uletaji wa mafuta. Lakini ziko sababu lazima ziangaliwe kwa undani ambazo zitasaidia kupunguza mzigo kwa wananchi.

”Tuangalie kuna vitu tunadhani bei zake zimekuwa kubwa zaidi ni kazi ya Ewura kupitia kufanya utafiti kujiridhisha kama hizo chaji ni halisi, tumekubaliana na Ewura na wakala wa Uagizaji mafuta kwa pamoja na wizara ya nishati tutapitia bei upya premium zote tunazotumia kuagiza mafuta ili tupate bei halisi mafuta ili Watanzania waweze kupata nishati kwa bei nafuu ia sisemi tunapunguza bei ya mafuta wala ninachosema tunapitia tujiridhishe na bei kama tumeambiwa ni bei kadhaa je ni bei hiyo halisi?” amesema Dkt. Biteko

Naibu Waziri Mkuu amesisitiza kuwa timu itafanya hiyo kazi. Suala la upangaji wa bei Ewura kuwa ni jambo linalowapa simanzi wananchi kila wakati bei inapotaka kubadilika, mafuta yanaadimika baadaye mafuta yanaanza kupatikana huo ndio mchezo watanzania hawawezi kufanyiwa lazima wafanyabiashara wajue pamoja na leseni ya biashara wanayopewa lengo lao ni faida na kukuza mtaji wao,lakini wahudumie Watanzania ili shughuli za uchumi zisitatizike siyo kuwaumiza.

Hata hivyo amewaomba wafanyabiashara wajue nao wanawajibu wa kuisaidia serikali kwa leseni walizopewa wafanye kwa uaminifu kwani kiwango cha uagizaji mafuta kimepungua lakini serikali imechukua hatua za haraka kuhakikisha kuwa hilo pengo linashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Sanjari na hayo Dkt Biteko amebaini kuwa ziko taarifa za watu wachache humo ndani ya EWURA wasiowaaminifu wanajihusissha na vitendo vidogo vidogo kwani wakitaka kufanya operasheni mtaona wahusika wote mnaotaka kufanya operesheni wana taarifa siku hiyo hiyo.Alafu kesho wote wa dharura.

“Kwenye tatizo la mafuta mnaenda kukagua mnakuta vituo vimefunga na hawapo,kwa nini ndani ya EWURA kuna watu wanataarifa hizo na wanaenda kuwaambia wanazivujisha na kufanya ukaguzi uwe mgumu.” amesema Naibu Waziri

Aidha wito umetolewa kwa EWURA kama mdhibiti kuanza kupitia mfumo mzima wa upangaji wa bei kuona kama bei tunazopanga zinakwenda na hali halisi kama kuna shida ya mafuta kutoka kwa wazalishaji wakubwa lakini mahitaji ya mafuta yameongezeka kwa sababu shughuli za kiuchumi zimeongezeka

Watu wanajenga viwanda mahitaji ni makubwa ya mafuta lazima tufikiri jinsi ya kuziba hilo pengo hilo

Sasa Serikali inampango mkakati wa LNG

Magari yanayotumia gesi asilia, kwanini tusiyaongeze. Ewura tuanze na mpango huo ili magari yanatotumia gesi asili yawe mengi zaidi na tupunguze matumizi ya mafuta tuhame kutumia mafuta twende kwenye gesi

“hili linawezekana kama sote tutakubaliana tuhame kwenye magari yanayotumia matufa twende kwenye gesi na tuanze na magari ya serikali tubadilishe mfumo wake kwenda LNG tujenge vituo vingi vya LNG

\Tukipunguza hiyo volume ya magari tutapunguza mafuta yanayofutmika mengi yatatumika kwa viwanda” amesisitiza Dkt Biteko

Aidha Naibu waziri Mkuu Doto Biteko ametoa maelekezo kama taasisi ya udhibiti ni lazima wafanye kazi kama timu moja, mitawanyiko huyo wa nani huyo wa fulani haitakiwa hata kufikiriwa, lazima watu wawe professional wafanyw vitu vyao kitaaluma na kwa mujibu wa sheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!