Mgeni rasmi katika kilele cha Maadhimisho ya Kimataifa ya Usalama na Afya mahala pa kazi , Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Doto Biteko akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Afya na Usalama mahala pa Kazi wa Kampuni ya Tigo Bwn. Dismas Anthony , kuhusu namna Tigo inavyoshirikiana bega kwa bega na serikali katika kuhakikisha usalama wa wafanyakazi kuwa ni jambo linalopewa kipaumbele , kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Kazi , Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi.