Home Kitaifa NAIBU KATIBU MKUU MADINI ASISITIZA KASI YA UJENZI WA JENGO JIPYA LA...

NAIBU KATIBU MKUU MADINI ASISITIZA KASI YA UJENZI WA JENGO JIPYA LA WIZARA MTUMBA

#Jengo jipya la Wizara ya Madini, Mji wa Serikali Mtumba wafikia asilimia 58.59

#Ampongeza Rais Dkt. Samia kwa kutoa fedha ukamilishaji miradi

#Wafanyakazi kupata mazingira bora ya kufanya kazi jengo likikamilika

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo amemtaka Mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuongeza kasi ya ujenzi wa jengo jipya la wizara ili mradi huo ukamilike katika muda uliopangwa wa kipindi cha miezi 18.

Mbibo amesema hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa ofisi mpya za Wizara katika mji wa Serikali – Mtumba leo Februari 1, 2023 Jijini Dodoma

Amesema, wizara imetoa msukumo kwa mkandarasi huyo wa mradi na mshauri ili iweze kufanya kazi kwa kasi zaidi na mradi ukamilike kwa wakati katika muda uliopangwa.

Akizungumzia kuchelewa kwa mradi huo kwa siku 28 amemsisitiza mkandarasi na mshauri kufidia muda uliochelewa wa ujenzi ili kufikia tarehe 14 Aprili 2023 mradi ukamilishwe.

“Tumekuja kuangalia uhalisia wa hatua za ujenzi ambazo zimefikiwa ili kuweza kulinganisha na taarifa ambazo wizara inapokea wizarani na kuijadili na kuangalia namna ya kutoa maamuzi sehemu zilizokwama,” amesema Mbibo.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Meneja wa Mradi kutoka NHC Nelson Novath amesema, mradi umetoa ajira 162 hadi sasa na wanatarajia kutoa ajira 60 ili kuongeza ufanisi na kufidia muda waliochelewa ili jengo hilo likamilike kwa wakati.

Ziara hiyo imehudhuriwa na Wajumbe wa menejimenti, baadhi ya watumishi wa wizara, na uongozi wa NHC ili kujionea maendeleo ya mradi huo. Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu.

##########

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!