Home Kitaifa MWITIKIO WA KAULI YA WAZIRI AWESO, MIPAKA YAIMARISHA HIFADHI YA MAKUTOPORA

MWITIKIO WA KAULI YA WAZIRI AWESO, MIPAKA YAIMARISHA HIFADHI YA MAKUTOPORA

Maelekezo ya Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) kuhusu kuhifadhi na kuendeleza vyanzo vya maji hapa nchini kwa kuwashirikisha viongozi na wananchi yameshika kasi na kufanikishwa katika eneo la hifadhi ya Makutopora, Jijini Dodoma.

Waziri Aweso alitoa maelekezo hayo hivi karibuni katika kikao kazi na watendaji wa Sekta ya Maji ambapo alisisitiza ili huduma ya maji iwe endelevu upo umuhimu wa dhati kwa kila kiogozi na wananchi kushirikishwa katika kazi ya uhifadhi.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabbir Shekimweri, kufuatia hilo ametembelea eneo la hifadhi ya maji chini ardhi – Makutopora na kukagua utekelezaji wa maagizo ya shughuli za uhifadhi wa eneo hilo zinazoendelea.

Mhe. Shekimweri amekagua njia zilizochongwa kwa ajili ya kuzuia adhari za moto zenye urefu wa kilometa 22, alama za mipaka kuonyesha mwanzo wa hifadhi na mwisho wa hifadhi pamoja na kukagua alama za kudumu za mipaka (beacon).

Mhe. Shekimweri ameridhishwa na utendaji kazi uliofanyika ikiwamo ujenzi wa alama za kudumu zenye ukubwa wa mita mbilizinazoonekana jambo litakalosaidia kupunguza uvamizi kwa visingizio vya kutokufahamu eneo ni la hifadhi.

Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Dodoma imetoa pongezi kwa ubunifu wa njia zilizochongwa kwasababu zimekidhi viwango vya uzuiaji wa moto hivyo kero za moto kushambulia eneo kubwa zitapungua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!