Home Kitaifa MWILI WA DIWANI CHARLES MWITA KUPUMZISHWA IJUMAA

MWILI WA DIWANI CHARLES MWITA KUPUMZISHWA IJUMAA

Na Shomari Binda-Musoma

MWILI wa aliyekuwa diwani wa Kata ya Mshikamano iliyopo manispaa ya Musoma,unatarajiwa kupumzishwa kwenye makazi yake ya milele ijumaa julai 14

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Musoma Benedict Magiri amesema maandalizi ya shughuli za mazishi yanaendelea vizuri kwa kushirikiana na familia.

Amesema jana jumanne walipokea mwili wa marehemu kutoka Dodoma kwenye hospital ya Benjamin Mkapa alikokuwa akipata matibabu na kuhifadhiwa hospital ya rufaa ya mkoa wa Mara.

Magiri amesema leo jumatano mwili wa marehemu utalala nyumbani kwake Kata ya Mshikamano na kesho alhamis utaagwa na kuelekea kijiji cha Bitaraguru kwaajili ya mazishi.

Amesema Chama cha Mapinduzi wilaya ya Musoma kimempoteza kada wake ambaye alikuwa na mapenzi makubwa na Chama hicho.

Mwenyekiti huyo wa CCM wilaya ya Musoma amewaomba wanachama wa chama hicho na wananchi wote kushiriki kikamilifu msiba huo hadi watakapo mpumzisha kwenye makazi yake ya milele.

“Tumempoteza ndugu yetu Mwita tukiwa bado tunahitaji mchango wake kama chama na wananchi wa Kata ya Mshikamano kama diwani wao”

Haya ni mapenzi ya Mungu na hii ni safari ya kila mmoja na niwaombe wana CCM na wananchi wote tushiriki kikamilifu kwenye msiba huu“,amesema Magiri.

Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amefika nyumbani kwa marehemu,Charles Mwita na kusaini kitabu cha maombolezo na kusema wataendelea kukumbuka mchango wake hasa kwenye vikao vya chama na baraza la madiwani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!