Home Kitaifa MWENYEKITI WA CCM PWANI ATAKA STAHA KUWAONYA VIONGOZI WA SERIKALI WAKIKOSEA JAMBO

MWENYEKITI WA CCM PWANI ATAKA STAHA KUWAONYA VIONGOZI WA SERIKALI WAKIKOSEA JAMBO

•VIONGOZI WA SERIKALI WASIUMBULIWE HADHARANI – MLAO

Na Scolastica Msewa, Kibaha

Mwenyekiti wa CCM Mkoani Pwani Mwinyishehe Mlao amewataka Wajumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Pwani kuzingatia katiba ya CCM kwa kutumia busara kuwaonya, kuwarekebisha viongozi wa serikali badala ya bila staha mbele za watu.

Amesema hayo mjini Kibaha wakati akifunga Kikao cha kawaida cha halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Pwani amesema Viongozi wa Chama na serikali wote ni viongozi nao ni viongozi kama wao wanastahili heshima.

Amesema inawezekana Viongozi wa serikali wakawa wamekosea lakini ni lazima kuangalia kiongozi huyo wa serikali anajadiliwa wapi na unazungumza nae wapi maana kila mtu anastahili heshima ya kuthaminiwa utu wake.

Mlao amesema katiba ya CCM imeweka wazi hilo hata kama kiongozi huyo wa serikali anakosea sana lakini usimuumbue bali muite zungumza bar.

“Kila mtu hapendi kuumbuliwa hata kama kiongozi huyo anaweza kukuambia jambo na wewe ukaelewa kabisa kwamba kiongozi huyo anakuongopea kuwa na hekima tulia baadae kwa busara ndipo umweleze ukweli unaoufahamu hapo hamtagombana mtakuwa kitu kimoja na mtamapiza shughuli za Chama na serikali mkiwa salama”

“Hata kama kiongozi huyo anatabia za ujana nyinyi kaeni nae vizuri maana Kuna hatima ya Kesho mwambie yupo hapo unafanya kazi za CCM na viongozi wa CCM ndio sisi tumieni hekima” amesema

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!