Na Scolastica Msewa, Chalinze.
Mwenyekiti Wa Bodi ya korosho Tanzania Brigadia General Mstaafu Aloyce Mwanjile amesema anampango wa kuanzisha shamba darasa la korosho katika Shule ya Sekondari ya Kimange huko Chalinze mkoani Pwani kwa lengo la shule hiyo ijiimarishe kiuchumi sambamba na kutoa elimu ya kilimo cha korosho kwa Wanafunzi mkoa wa Pwani.
Amesema hayo wakati akihutubia katika mahafari ya Kumi ya Shule hiyo ya Sekondari ya Kata ya Kimange Chalinze mkoani Pwani ambapo alikuwa Mgeni rasmi.
Brigadia General Mstaafu Mwanjile amesema kilimo cha korosho ni miongoni mwa mazao yanayoweza kuwakwamua vijana nchini kiuchumi hivyo aliwasisitiza wahitimu wa Shule hiyo kufanya kazi kwa bidii hususani kilimo cha korosho ili waondokane na umasikini wa kipato.
Amesema ameipenda shule hiyo ya Sekondari ya Kimange na kuahidi kuwa rafiki wa karibu wa Shule hiyo ambapo ameahidi pia kutoa shilingi lakini Tano kwaajili ya Walimu ambao masomo yao Wanafunzi watapata ufaulu wa daraja la kwanza ‘A’ na shilingi laki Moja kwaajili ya Kila daraja la kwanza ‘A’ “division one” la Kila mwanafunzi atakayepata.
“Tuingie mkataba na Walimu, niwaombe kuanzia Leo Mimi ni rafiki wa hii Shule Mimi baada ya kustaafu jeshi nimekuwa mkulima wa korosho na bahati nzuri Rais Dkt. Samia ameniteua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya korosho Tanzania Sasa kwakuwa Mimi ni mkulima ni waahidi Walimu watakaohusika kwenye hizo ‘A’ kutakuwa na motisha na kwa kuanzia natenga shilingi laki tano” amesema.
“Maana ili Walimu waweze kufanya kazi yao vizuri lazima tuweke motisha uongozi utaona namna ya kuwapatia waliosababisha hizo ‘A’ kwa Wanafunzi Kila Division one Kuna laki Moja yaani Kila Division one itakayopatikana Kimange Sekondari nidaiwe laki moja nafanya hivyo kwa makusudi ili muongeze jitihada”
Aidha pia ameahidi kuwanunulia laptop Moja kwaajili ya shughuli za Ofisi za kufundishia Wanafunzi shuleni hapo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari ya Kimange Ramadhani Kabelwa amewataka Wazazi kuhakikisha wanafika Wanafunzi wanarudi shule kuendelea na masomo mara baada muda wa likizo unapokwisha ili waweze kuendelea na masomo yao.
Aidha amehimiza uimalishaji wa elimu ya msingi nchini ili Wanafunzi wakidhi mahitaji ya elimu ya Sekondari “wanakuja Wanafunzi kutoka shule za msingi lakini uwezo wao unakuwa bado ni mdogo kiasi kwamba Walimu wa Sekondari hulazimika kufanya kazi ya ziada ambayo ilitakiwa ifanywe na shule za msingi na kusababisha kuchelewa kwa Maendeleo ya wanafunzi hao katika ngazi ya Sekondari.
Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kimange Wema Mbwana amesema Shule hiyo Ina eneo la kutosha la zaidi ya hela mia Moja ambazo zinaweza kutumika kwaajili ya shamba Hilo darasa la zao la korosho kwa Wanafunzi hao.
Hatahivyo ameshukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha Shule hiyo inapata miundombinu ya kutosha ikiwa ni pamoja na vyumba vya madarasa, bwalo la chakula, maabara ya kufundishia moja kwa masomo ya sayansi.
Aidha amesema Shule hiyo bado Kuna changamoto ya utoro kwa Wanafunzi hali ambayo hupelekea Wanafunzi wengine hata kuacha kabisa shule jambo ambalo hutokana na Wazazi kutokutoa ushirikiano kwa uongozi wa Shule katika kuwasaidia Wanafunzi wao shuleni hapo.
“Wazazi wamekuwa wagumu kwenye elimu na wanamwamko mdogo kwenye kuhamasisha elimu” amesema Mwalimu Wema.
++++++++++++++