Home Kitaifa MWENYEKITI UWT MKOA WA MARA NANCY MSAFIRI AMPONGEZA MBUNGE AGNESS MARWA ZIARA...

MWENYEKITI UWT MKOA WA MARA NANCY MSAFIRI AMPONGEZA MBUNGE AGNESS MARWA ZIARA YA VIONGOZI ZANZIBAR

Na Shomari Binda

MWENYEKITI wa UWT mkoa wa Mara Nancy Msafiri amempongeza mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Agness Marwa kwa kuwaandalia ziara maalum viongozi wa UWT kutoka mkoani Mara hadi visiwani Zanzibar.

Ziara hiyo ya viongozi hao kutoka wilaya zote za mkoa wa Mara iliyopewa jina la Mara To Zanzibar Royol Tour imehitimishwa Siku ya jana kwa mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Muyuni wilaya ya Kusini Unguja.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wakazi wa wadi ya Muyuni kizimkazi alipozaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Licha ya wananchi mkutano huo ambayo mgeni rasmi alikuwa Nancy Msafiri umeudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Mnec) Mustapha Mvita, Mjumbe wa Baraza Kuu Wazazi Taifa Ndg. Shabani, Mkuu wa Wilaya ya Kusini Mh. Mkasaba, Katibu wa Ccm Wilaya Ya Kusini, Madiwani, Wajumbe wa kamati za Siasa Wilaya, Kata na Tawi, na Viongozi wengine mbalimbali waliopata gursa ya kutoa salam zao.

Nancy Sesani Msafiri amempongeza mbunge Agnes Marwa kwa ubunifu wa hali ya juu kuwapeleka wanawake wa Mara Zanzibar huku akimtaka kuwa na amani kwa kuwa ziara ya viongozi aliyoiandaa ina baraka zote kutoka kwa viongozi UWT Taifa Chini ya Mwenyekiti wake Marry Chatanda.

Amesisitiza kuwa ziara hiyo imekua ya mafanikio makubwa kwa maslahi mapana ya Muungano.

Nae diwani wa Wadi ya Muyuni Pochi Pochi amewataka wana Mara kuendeleza udugu na umoja ulioanzishwa na mwana Mara namba moja ambaye pia ni Baba wa Taifa Mwl. Jk Nyerere na Hayati Amani Karume katika pongezi hizo amesema Wana Mara wameacha deni ambalo hawajui watalilipa vipi.

Kwa upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara Agness Marwa amesema wataendelea kuwaunga mkono Rais Dkt.Samia na Dk.Hussen Mwinyi kwa jitihada zao za kuwaunganisha watanzania na kuwaletea maendeleo.

Mara to Zanzibar Royal Tour imekamilika kwa kukamilisha Wilaya zote saba za Mkoa wa Mara ambapo wajumbe wa Baraza la Uwt Mkoa mzima wamepata fursa ya Kwenda Zanzibar na kutembelea vivutio mbalimbali pia wametembelea Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kujifunza namna linafanya kazi.

Ziara hiyo iliandaliwa na mbunge Agnes Marwa kwa lengo la kutangaza Utalii wa Ndani ikiwa ni kuunga mkono juhudu za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Royal Tour lakini pia kudumisha Muungano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!