Home Kitaifa MWENYEKITI UWT ILEMELA KUTEMBELEA KATA 19 KUWAJENGEA KINA MAMA UWEZO

MWENYEKITI UWT ILEMELA KUTEMBELEA KATA 19 KUWAJENGEA KINA MAMA UWEZO

Na Neema Kandoro Mwanza

Kamati ya Siasa Wilaya ya llemela ikiongozwa na Mwenyekiti wa Wanawake Wilaya ya Ilemela (UWT) Salome Mtambalike wanafanya Ziara ya Kata 19 Lengo ikiwa ni kuhakikisha Wanawake wanajitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi na kuwajengea uwezo wa kujiamini.

Mtambalike amewataka pia Wanawake kutokua waoga wa kuchukua hatua ya kutatua migogoro mbalimbali ya wakina Mama katika maeneo yao.

Alisema migogoro imekuwa ikichelewesha maendeleo mathalani Kata ya Kitangiri inachelewa kupata maendeleo kwa sababu ya migogoro ambayo inaendelea.

Mtambalike alisema tunaona Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani ni Mwanamke na amekuwa mfano wa kuigwa kwani kashika nafasi ya Urais hivyo basi nanyi Wanawake msilale amkeni.

Lakini pia Katibu wa UWT wilaya ya Ilemela Arafa Njechele alisema ziara hiyo inalenga pia kuwapa Elimu Wanawake kuhusu Ukatili kwa sababu wanawake wengi wamekuwa waoga kwenye kutoa taarifa pindi matatizo ya kikatili yanapokuwa yanajitokeza hivyo hii ni ziara muhimu sana kwa wakina Mama .

Alisema kuna haja ya kuwahamasisha pindi tutakapokuwa kwenye kata jitahidini kujitokeza nyie wanamke kwani kuna mambo mazuri ya kugawa kadi za Chama Cha Mapinduzi CCM hivyo Kila Mwanamke hakikisha uwe na kadi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!