Home Kitaifa MWENYEKITI HANCY, DIWANI ASHA MUHAMED WACHANGIA TOFALI 250 UJENZI NYUMBA YA KATIBU...

MWENYEKITI HANCY, DIWANI ASHA MUHAMED WACHANGIA TOFALI 250 UJENZI NYUMBA YA KATIBU UWT MUSOMA

Na Shomari Binda-Musoma

MWENYEKITI wa ( UWT) mkoa wa Mara, Nancy Msafiri, na diwani wa viti maalum manispaa ya Musoma Asha Muhamed wamechangia tofali 250 kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT Musoma mjini.

Akiwa ameongozana na wenyeviti na makatibu Kata wa (UWT) wilaya ya Musoma mjini, diwani wa viti maalum manispaa ya Musoma Asha Muhamed, amesema kama diwani amewiwa kuchangia ujenzi huo.

Amesema mtumishi kama Katibu akipata makazi na kutulia ataweza kufanya majukumu yake bila wasiwasi.

Asha amesema kwa upande wake alisha changia mchango wa jumla na madiwani wengine wa viti maalum na ameamua kuchangia tena tofali 100.

Leo nimekuja tena na viongozi wangu wa Kata kuchangia tofali nyingine 100 kwaajili ya kuendeleza ujenzi laki zipo pia tofali 150 za Mwenyekiti wetu wa mkoa Nancy Msafiri”,amesema Asha.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa mkoa wa Mara(UWT),Mjumbe wa baraza la wazazi mkoa toka UWT,Shani Hamisi,amesema Mwenyekiti Nancy analidhidhwa na kasi ya ujenzi na ameamua kuunga mkono.

Amesema Mwenyekiti anawashukuru viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge wa viti maalum kwa namna wanavyochangia ujenzi huo.

Katibu wa (UWT) Musoma mjini, Angel Simwanza na Mwenyekiti wake,Stela Mtani,wamemshukuru diwani Asha Muhamwd na Mwenyekiti, Nancy Msafiri,kwa mchango wao wa tofari 250 kwaajili ya ujenzi wa nyumba ya mtumishi.

Aidha wamewashukuru viongozi wa Kata wa UWT kwa kutoa fedha za mafundi tangu ujenzi huo ulipoanza hadi sasa unapoendelea.

Kwa upande wao viongozi wa Kata ( UWT) waliokuwepo kwenye makabidhiano ya tofali hizo,wamemshukuru diwani,Asha Muhamwd na Mwenyekiti wa mkoa kwa mchango wao na kuwaomba viongozi wengine na wanachama wa CCM na jumuiya zake kujitokeza kuchangia ujenzi huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!