Home Kitaifa MWENEZI MAKONDA ATOKWA NA MACHOZI

MWENEZI MAKONDA ATOKWA NA MACHOZI

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda ametokwa na machozi mara baada ya kusikia malalamiko ya Mwanamama mkazi wa Tinde Mkoani Shinyanga ya kutekewa mmewe na kudhulumiwa shamba lake tangu mwaka 2021 na hakuna haki stahiki yoyote iliyotendeka kwake.

Hayo yamejiri wakati Mwenezi Makonda aliposimama eneo la Tinde na kusikiliza kero za Wananchi hao akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya Mikoa 20 Back To Back.

Mbona Polisi mnawaonea sana watu maskini, mtu ametekwa miaka mitatu iliyopita, eneo lake limechukuliwa na mtuhumiwa mnayemjua na kujengwa kiwanda lakini hamchukui hatua yoyote Mwenezi Makonda.

Basi kama mnashindwa kumtafuta mtu aliyetekwa, mmeshindwa hata kutenda haki kwa kumrudishia eneo lake ambalo Takukuru imethibitisja kwamba wanalimiki kihalali mjane wake? Hapana msifanye hivyo Mwenezi Makonda.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kuitambua kesi hiyo na kubainisha kuwa Jalada la Kesi hiyo iliyofunguliwa miezi mitatu iliyopita lipo kwa Mwedesha Mashitaka Mkuu wa Serikali DPP.

Hoja hizo zimemfanya Mwenezi Makonda kushikwa na simanzi, kulia na kushindwa kuendelea kusikiliza kero za wananchi wa Tinde Mkoani Shinyanga na kuahidi kufuatilia jambo hilo ili haki itendeke kwa haraka kwa Mwanamama huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!