Katibu wa Halamshauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda akisalimiana na kuzungumza na Wananchi wa Kibondo Mkoani Kigoma.
Akiwa eneo hilo, Makonda amepokea malalamiko ya changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama.
Makonda ahoji lini maji yatapatikana ambapo Meneja wa Mkoa wa RUWASA amemuahidi Mwenezi Makonda kutatua changamoto hiyo kwa haraka
Aidha,Makonda amtaka Mkuu wa Wilaya ya Kibondo kuhakikisha ukamilishwaji wa visima viwili vya maji unafanyika kwa haraka ili wananchi kuondokana na changamoto ya maji.
Vilevile, Mwenezi Makonda amepokea changamoto zingine mbalimbali zilizogusaia masuala ya ardhi.