Home Kitaifa MWEKEZAJI MAFUTA ALIZETI AWATAKA WAKULIMA KUONGEZA UZARISHAJI,ALIA UHABA WA MALIGHAFI

MWEKEZAJI MAFUTA ALIZETI AWATAKA WAKULIMA KUONGEZA UZARISHAJI,ALIA UHABA WA MALIGHAFI

Na Boniface Gideon, MARA

Mwekezaji wa kiwanda chakuchakata zao la Alizeti Nyihita Wilfred mwekezaji amewaomba Wakulima wa zao Hilo kuongeza uzarishaji wa zao Hilo ili kukidhi mahitaji ya Kiwanda ,
Mwekezaji huyo mzawa aliyejikita kwenye sekta ya kilimo kupitia zao la Alizeti katika Kijiji Nyanchabakenye Wilaya ya Rorya mkoani Mara ambapo sasa amekuwa mwarobaini kwa wakulima wengine ambao wamepata soko la kuweza kuuza mazao yao baada ya kuanzisha kiwanda cha kuchakata zao hilo la mafuta Nyihita Sunflower Cooking oil Production.

Akizungumza Jana na Waandishi wa Habari, Nyihita alisema mahitaji ya Kiwanda hicho kwa Siku ni Tani 24 lakini kwasasa wanapata asilimia 5 tu ya mahitaji ya Kiwanda alichokijenga kwaajili ya kuchakata zao hilo na kuwa mzalishaji mkubwa wa mafuta yayokanayo na Alizeti lakini pia ameweza kufungua na kutoa ajira kwa vijana hatua ambayo ni ya kujivunia kwa Wakazi wa Wilaya hiyo.

Mwekezaji huyo alisema aliigeuza changamoto na kuwa fursa kwake hii ni kutokana na kukosekana kwa kiwanda cha zao la Alizeti ndani ya mkoa huo na hivyo kupata wazo la kuja na sasa ana miliki kiwanda cha kuzalisha mafuta ya kula yatokanayo na zao hilo alichokipa jina lake la Nyihita Sunflower Cooking oil Production.

Nilipata wazo la kuja kufanya uwekezaji wa kilimo cha Alizeti ndani ya mkoa wa Mara ikiwa ni eneo ambalo halikiwahi kuwa na historia ya kilimo cha Alizeti na niliamini kwamba malighafi zinapatikana kijijini na maendeleo makubwa na mapinduzi ya viwanda yanafanyika vijijini.

“Nialiamua kuja vijijini ambako niliamini ninaweza kuja kuwashawishi wakulima ambao mashamba yapo ili waweze kulima na ni kweli wazo hili lilifanikiwa kwa asilimia 100 kwani wakulima walijitokeza na kuanza kulima kilimo cha Alizeti mwaka 2019, na ilipofika 2020 wakulima walianza kujiuliza maswali mara baada ya kulima mazao tutauza wapi nikapata wazo kwa kutafuta wazo la soko na kujenga kiwanda baada ya kuanza ujenzi huo kiwanda hiki kilizinfuliwa rasmi 2021 na kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa na ndio kikaanza kufanya kazi mpaka sasa” alisema

Alisema anajivunia kuwa Mwekezaji mzawa na mmoja wa watanzania ambao wanaweza kuzalisha fursa za ajira kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo sambamba na kuwapatia soko la uhakika wakulima hatua ambayo imekuja kuleta mwamko wa wakulima wengi kujikita shambani tofauti na ilivyokuwa awali.

Pamoja na hayo uwepo wa kiwanda hiki kimeweza kutengeneza fursa za ajira kwa vijana wetu wa kitanzania lakini pia kuongeza uchumi wa mtu mmoja mmoja kwahiyo tumeongeza wigo mpana kwa ndugu zetu wa Mara kuweza kuongeza pato lao kupitia kiwanda hiki na wakulima kuweza kupata soko la uhakika na kuuza malighafi zao hapa na pia kiwanda hiki kimeweza kuwa faida kwa nchi yetu ya Tanzania kwani tunalipa kodi na zinasaidia kuleta maendeleo kwenye Taifa letu” aliongeza mwekezaji huyo.

Ni wito wangu kwa watanzania na wana Mara kujikita kwenye kilimo cha Alizeti wakitumie kama fursa na kuhakikisha tunasaidia kuinua uchumi wa Taifa letu lakini pia kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja ndani ya Tanzania kwa ujumla” alisisitiza.

Nyihita alisema ukubwa wa kiwanda hicho hauendani sawa na mali ghafi inayozalishwa mashambani ambayo imekuwa ni mdogo hatua ambayo amewaasa wananchi kuendelea kujikita katika kilimo hicho kwani tayari uhakika wa wapi watauza mazao yao upo ni suala tu la kuongeza uzalishaji.

Uwezo wa kiwanda ni mkubwa tofauti na Malighafi inayoweza kupatikana, kwa misingi hiyo basi tunahitaji wakulima wajitokeze kwa wingi kulima wakijua kwamba fursa ya soko la uhakika ipo ili waweze kusaidia kiwanda kuweza kuzalisha kwa wingi na kupata ukamilifu wa uhitaji wa mali ghafi

“Sasa hivi wizara ya kilimo imeanzisha kilimo biashara wazo hili linasaidia vijana wakitanzania na watanzania kwa ujumla kuweza kujikita kwenye kilimo kwahiyo kupitia wazo hili la kilimo biashara litasaidia watanzania kujiwekeza ni matumaini yangu kwamba kupitia kilimo biashara vijana wengi watajitokeza kulima zao hili ambalo litasaidia kuongeza utoshelevu wa uhitaji wa malighafi” Alisema

Mariam Hamis ni miongoni mwa wakulima na wanufaika wakubwa wa zao la Alizeti Alisema wamekuwa wakijihusisha na uzarishaji wa zao Hilo kwa muda mrefu lakini hawakuwahi kupata mafanikio kutokana na kukosa soko hivyo kwasasa wanashukuru uwepo wa kiwanda hivyo

tumekuwa tujihusisha na kilimo Cha kawaida tu katika zao hili ili tupate pesa kwaajili ya kukidhi mahitaji ya familiya lakini hata hivyo tumekuwa na changamoto ya muda mrefu wa kupata soko la uhakika kwajili ya kuuza mazao yetu yalikuwa yanaharibika.

“Lakini kwa sasa uwepo wa kiwanda hiki ni furaha kwetu wakulima kwasababu tayari tumepata uhakika wa kutosha kuhusu changamoto ya muda mrefu, tulikuwa hatujui ni wapi tutauza mazao yetu baada ya kuvuna, tunashukuru Sana mwekezaji kwa kuona changamoto hii na kuitatua katika wilaya yetu na sasa wakulima wote tumehamasika na tunanufaika vyakutosha na uwepo wa kiwanda hiki

Alisema Vijana Wengi hususani wa vijiji vinavyozunguka eneo la Kiwanda hicho wamepata mwamko mkubwa wa kufanya kazi hususani za Kilimo kutokana na uhakika wa soko la Alizeti,

Vijana wengi tunafaidika na kunufaika na uwepo wa kiwanda hiki kutupatia ajira ambapo watu waliosoma na wasio soma wameweza kuajiriwa katika kiwanda cha Nyihita Sunflower Cooking oil Production na kimeweza kupunguza upungufu wa ajira ambalo ni tatizo bado katika nchi yetu, uwepo wa kiwanda hiki umekuwa na manufaa kwa wananchi wengi” Alisema Mariam

MWISHO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!