Home Michezo MWANZA VETERAN MABINGWA NYERERE DAY BONANZA 2023

MWANZA VETERAN MABINGWA NYERERE DAY BONANZA 2023

Na Shomari Binda-Musoma

TIMU za soka na netball za Mwanza veteran zimechukua ubingwa wa bonanza la Nyerere day 2023 lililoitimishwa mjini Musoma.

Kwenye upande wa soka Mwanza veteran wamechukua ubingwa kwa kuifunga timu ya Musoma veteran mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali.

Kwenye mchezo wa netball Mwanza veteran wamekuwa mabingwa kwa kuwafunga Musoma Queen point 40 kwa 22

Mwanza veteran tangu mwanzo wa bonanza hili la kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere oktoba 14 walionekana kuja Musoma kuchukua ubingwa.

Nidhamu kubwa ya kiuchezaji kwa timu zote za soka na netball ilionekana bayana kutafuta jambo msimu huu.

Kwenye mchezo wa soka Mwanza veteran waliwavua ubingwa Rock City veteran kwenye mchezo wa nusu fainali kwa kuwatoa kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-3 huku kwenye netball wakitetea ubingwa waliochukua mwaka jana.

Akifunga bonanza hilo mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda amewapongeza Mwanza veteran kwa kuwa mabingwa kwa michezo yote msimu huu.

Amesema kufanya mazoezi na kujitunza kwa watu wazima ndio lengo la kufanya vizuri kwenye mashinsano ya veteran.

RC Mtanda amesema katika mashindano ya mwakani waratibu wanapaswa kuandaa vizuri zaidi na kufanya bonanza hilo kuwa bora.

Mwenyekiti ws Musoma veteran ambao ndio waandaji wa bonanza hilo wamewashukuru wadau wote waliochangia na kufanikisha kufanyika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!